ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
Msemaji wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kiongozi huyo huwa anapumzisha macho tu na si kulala wakati wa mikutano kama wanavyoamini watu wengi.
"Rais huwa anasumbuliwa na mwanga mkali," George Charamba amenukuliwa akisema na gazeti la serikali la Herald.
Rais huyo kwa sasa yupo nchini Singapore akipokea matibabu maalum kwenye macho yake.
Bw Mugabe, 93, anapanga kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
"Huwa najihisi kama mtu ambaye amekosa kutekeleza kazi yake vyema ninaposoma (kwenye vyombo vya habari na mtandaoni) kwamba rais alikuwa anasinzia katika makongamano - la hasha," Bw Charamba amesema.
Source: BBC Swahili