Msemaji wa M23 auawa kwa shambulio la drone

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
20260224_204032.jpg

Msemaji wa kijeshi wa kundi la M23, Willy Ngoma, ameuawa kwenye shambulio la ndege zisizo na rubani, katika eneo la Rubaya, wilayani Masisi- Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kwa mujibu wa BBC, ofisa mmoja wa kidiplomasia na ofisa mwengine mwandamizi wa kundi hilo la M23 wameiambia shirika la habari la Reuters kuwa Msafara wa Willy Ngoma na maafisa wengine wa M23 ulishambuliwa na ndege hizo zisizo na rubani.

Kifo cha Willy Ngoma kimejiri huku mazungumzo ya kusitisha mapigano yakiendelea nchini Qatar, huku serikali ya Congo, na M23 zikiwa zimesaini mkataba utakao idhinisha kuundwa kwa jopo litakalosimamia usitishwaji kwa mapigano utakaojumuisha waangalizi kutoka Qatar, Marekani na Umoja wa Afrika.

Kundi la M23 ambalo umoja wa mataifa unadai unaungwa mkono na Rwanda, linadhibiti eneo kubwa la mikoa ya kivu ya kusini na Kaskazini, kufuatia makabiliano makali kati yake na jeshi la serikali ya Congo FRDC, tangu mwaka wa 2024.

Vuguvugu la mto congo na M23 linadhibiti sehemu kubwa ya mikoa hiyo mbili na miji mikuu ya goma na Bukavu.

Shambulio lina linasemekana kutokea karibu na eneo la Rubaya, katika mkoa wa kivu ya kaskazini mwendo wa saa kumi za Usiku na limetokea siku kadhaa ambayo imehsuhudia mashambulizi ya anga katika eneo hilo.

Rubaya ni eneo la Kimkakati unaozalisha zaidi ya asilimia 15 ya madini ya Coltan duniani, na hivyo kuwa eneo muhimu kwa kundi la M23 kutokana na mauzo ya madini hayo.

Msemaji wa rais Felix Tshisekedi na msemaji wa jeshi la FRDC hawajasema lolote kuhusiana na tukio hilo au hata kuthibitisha kuhusika na mashambulio hayo ya ndege zizizo na rubani.

Hadi sasa uongozi wa vuguvugu la AFC/M23 halijathibitisha kuuawa kwa Willy Ngoma lakini tunaendee akufuatilia taarifa hizi kadri yanavyojiri.

Chanzo: BBC
 
View attachment 3548190

MBOKA NA NGAI sorry for your loss.
 
Safi sana na EL Mencho naye kala CHUMA ,ni mwendo wa kumaliza WAHUNI wanaoathiri binadamu.
 
Hii njia wanaitumia sana US na Israel, wanakutegea ukiwa unatoka Tu wanakuwasha, US ana satellite inayoweza kuona Hadi sindano ndogo au Pini kwenye ardhi hivyo wanakuwa wanajua Tu Hadi boksa uliyovaa au Hadi sehemu zako za siri kama umenyoa au lah, wanaomba wao ni ww kutoka tu utembee na gari au Kwa mguu lengo ni kupunguza uncessary casualties, attention sasa wanakuwinda tu kila siku, huyo aliingia 18 tena usiku ni muda mzuri WA kuuawa...siku hizi hata nchi za Afrika wanazo drone, baadhi zinazojitambua.
 
Ndiyo maana US walimpiga Ban DAB aka PCM kutokuingia USA kwa kuua raia.
 
Hii njia wanaitumia sana US na Israel, wanakutegea ukiwa unatoka Tu wanakuwasha, US ana satellite inayoweza kuona Hadi sindano ndogo au Pini kwenye ardhi hivyo wanakuwa wanajua Tu Hadi boksa uliyovaa au Hadi sehemu zako za siri kama umenyoa au lah, wanaomba wao ni ww kutoka tu utembee na gari au Kwa mguu lengo ni kupunguza uncessary casualties, attention sasa wanakuwinda tu kila siku, huyo aliingia 18 tena usiku ni muda mzuri WA kuuawa...siku hizi hata nchi za Afrika wanazo drone, baadhi zinazojitambua.

haha haujaonaleo tumetolea bastola hao US wako ...
 
Back
Top Bottom