Mkuu wetu na mwanachama mwenzangu. Kuna tetesi ambazo Leo zimekuwa gumzo mitaani kuwa Huyu mkurugenzi mwanadada Sanga ulimpa Ukurugenzi. Lakini bahati mbaya wakati unataka kuwaapisha, ukagundua kuwa siyo mwanachama mwenzetu. Lakini Juzi katika hotuba yako ulituhakikishia kuwa hukukurupuka kuwateua hao uliowateua. Ulisema ulihakiki jina kwa jina.
Swali langu ni je? Ni kweli umesitisha uteuzi wake kwa sababu siyo mwanachama wa chama chetu?
Swali la 2. Je? Ni kweli ulipitia jina kwa jina la kila uliyemteua na ukajiridhisha?
Najua wewe ni msomaji mzuri wa mitandao ya kijamii na Mara nyingi umekuwa ukijibu hata baadhi ya hoja hizo kupitia mikutano au hotuba zako. Ombi langu kwako ni ikiwa yaliyoandikwa na magazeti na mitandaoni ni ya kweli, Je? Unafikiri wananchi wanaokuombea Kama ulivyotuomba tukuombee tutajisikiaje?.
Mkuu, kumbuka maneno yako ambayo huwa unapenda kuyasema kila Siku nakunukuu
"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu" basi ikiwa ndiyo kumbuka pia ktk amri kumi za Mungu, kuna amri moja inasema usiseme uongo. Nakuomba ututengulie hiki kitendawili. Kumbuka baada ya uchaguzi kwisha na Raisi akapatikana kwa desturi ya nchi yetu huwa tunarudi kuwa kitu kimoja kwa maendeleo ya nchi yetu.
Ubaguzi wa namna yeyote uwe wa dini kabila au chama siyo kipaumbele kabisa katika mustakabali wa Taifa letu lenye matatizo kibao.Raisi wa nchi ya kidemokrasia ni Rais wa wananchi wote.na kwa kukumbusha tu Hilo, Mwenyekiti wetu JK kwa kuionyesha dunia ukomavu wa kisiasa, alimteu Mbatia kuwa mbunge wa viti maalum na kila mtu akijua kuwa Mbatia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR.