lidoda
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 641
- 574
Msema kweli kasema waziwazi kuwa hakuna ukame nchni na kwamba ni yeye tu atakaye tamka kama kuna ukame. Sasa huyu kiranja wetu wa mifugo na mazao, wakuu wa madhehebu wanasema kuna ukame. Hawa wakuu wa madhehebu wamefika mbali na kusema kuwa tuombee dua na tufunge kusudi tuepuke na janga hili.
Msema kweli vile vile kasema hakuna njaa na hakuna ukosefu wa chakula. Kiranja Mkuu na kiranja wa mifugo na mazao, Mamvi na Tindi, na Zit wanatuambia kuna jaa. Na kwamba kuna msosi mwingi sana ijapo hatujaonyeshwa hilo ghara la msosi.
Msema kweli kasisitiza hatagawa sembe, sababu yeye hana shamba na haijawahi kutokea waathirika kupewa msosi ktk hali kama hiyo, lakini yule kiranja mkuu, kiranja wa mifugo na mazao pamoja na Mamvi wana tupa moyo kuwa tusiwe na wasiwasi tutapata msosi.
Sasa mimi ningeomba kiranja wa maafandi uwaweke ndani hao wote wanaoenda kinyume na kauli ya Msema Kweli. Hawa ndio (Kiranja mkuu,kiranja wa mifugo na mazao, wakuu wa madhehebu, mamvi,Tind na Zit) wanaowagombanisha wadanganyika na msema kweli.
Kwa kufanya hivi wewe kiranja wa maafandi lazima utapandishwa cheo cha kuwa kiranja mkuu