MSEKWA: Hatuhitaji KATIBA MPYA

MSEKWA: Hatuhitaji KATIBA MPYA

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Asema "Sababu zilizolazimisha kuundwa mara mbili tangu uhuru kwa sasa hazipo"
Source : MWANANCHI gazeti la leo jtano june, 25, 2014
 
hawa ccm tulishasema wamefikia kikomo cha kufikiri, si wazee si vijana, akili zao wote sawa,
 
Nilivyomsikia Rais wangu alivyofungua Bunge nikajua hakuna kitu hapa, lakini ni vizuri akajitahidi kuacha kumbukumbu nzuri ya katiba na ujenzi wa barabara ya Arusha Musoma.
 
Kwa vile wanataka kutawala milele hawaoni sababu ya katiba mpya? Kwa vile wao wako huko juu na hawajui au hawaoni tulio chini tunavyoteseka kwa sababu ya katiba isiyokidhi? Wenyewe wangeifuata katiba iliyopo ingekuwa afadhali lakini wapi watu wanateswa, wanapigwa mabomu, wanavunjiwa makazi yao bila fidia wao wanaangalia. Wananchi wanalalamikia muundo wa muungano wao kimya! Mfumo mbovu wa serikali wa mawaziri kuwa wabunge wao wanauona sawa ili mawaziri wasiwajibishwe na mengine mengi tu as per Tume Ya Rasimu Ya Warioba!
TZ tunataka katiba mpya itawaamsha viongozi waliolala au wasiojitambua.
 
Ndungu watanzania wote mwenye macho haambiwi ona, ukawa waliwambia ccm wanavuluga upatikanaji wa katiba mpya sisi tunabisha! Sasa hiyo kauli ameongea wazi kuwa hawataki katiba mpya. Kweli katiba sio hitaji la watanzania? Tuyafanyeje haya majangili yanayo tumia pesa nyingi kwa katiba hewa?
 
Nchi hi watanzania tumezubaa mpaka basi,huyu mpuzi hakuwa na haki ya kupanua mdomo kusema hayo. Tumpe adhabu gani yeye na wahuni wenzie?
 
Kama uzee unafanya mtu kuwa hivi, bora ufe mapema kuliko kujidhalilisha kiasi hiki. Daima huwa nasema vijana kuwaachia wazee uongozi na kufanya maamuzi ni kama kukumbatia virus kwani hawa wazee hana dreams tena.

Mzee msekwa tunakuheshimu sana, bora ukae kimya kuhusu swala la katiba mpya. Istoshe wewe haitakuhusu sana maana umeshafika jioni, unachofikiria ni utalalaje?
====================================




msekwa_.jpg

Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa akikusanya baadhi ya vitabu alivyoviandika alipokuwa akifanya mahojiano na wahariri wa gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana. Picha na Mpoki Bukuku​


Dar es Salaam. Spika mstaafu, Pius Msekwa amesema haoni haja wala sababu ya msingi ya Tanzania kuandika Katiba Mpya kwa sasa kwani hakuna matukio makubwa ya kisiasa nchini yanayolazimisha kufanya hivyo.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam jana, Msekwa alisema hata hivyo, anakubaliana na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuruhusu kufanyika kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu alikuwa na sababu zake na alikwishazieleza wazi.

Alisema, "Sioni haja ya kuwa na Katiba Mpya. Mnatunga Katiba Mpya kama kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa, yaani mabadiliko ya kiutawala," alisema.

Alifafanua Katiba ya Tanganyika na hata ya Tanzania ilibadilishwa pale palipokuwa na matukio makubwa ya kiutawala, lakini pia kuna matukio mengine ambayo hayakulazimisha kuandikwa upya kwa Katiba.

Msekwa aliyeshiriki michakato yote ya katiba zilizotangulia ikiwamo hii ya sasa, alisema kwa kawaida Katiba Mpya inaweza kuandikwa panapokuwa na mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini kama ilivyotokea mwaka 1962 baada ya Tanganyika kupata uhuru wake, lakini Malkia wa Uingereza akaendelea kuwa mkuu wa nchi.

"Katika mazingira hayo Watanzania hawakujua maana ya uhuru ni nini, ikaleta sintofahamu, ikabidi Mwalimu (Julius Nyerere) na wenzake waamue kufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa kutoka kuwa chini ya Malkia kwenda kwa uongozi wa wananchi,'' alisema.

Pia, alieleza kuwa kuanzishwa kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilikuwa tukio jingine kubwa na la msingi lililosababisha kuandikwa kwa Katiba Mpya ya mwaka 1977.

"Mfano wa pili tulipoingia katika Muungano mwaka 1964, hapa kulikuwa na nchi mbili ambazo ni sovereignty (nchi zenye utawala kamili) tukaziunganisha, mazingira kama hayo yalidai Katiba Mpya.

Hata hivyo, Msekwa alisema hata mabadiliko kama ya mwaka 1965 kutoka mfumo wa vyama vingi vya siasa kuingia chama kimoja licha ya kuwa tukio kubwa, hayakulazimisha kuandikwa kwa Katiba Mpya, bali iliyokuwepo ilifanyiwa marekebisho.

Alisema tukio jingine ni la mwaka 1984 ambako mabadiliko mengine yalifanyika katika Katiba kwa kuingiza kipengele cha haki za binadamu na ukomo wa kipindi cha urais kuwa wa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja ambalo halikuhitaji Katiba Mpya.

Badiliko jingine kubwa ambalo halihitaji katiba mpya, Msekwa alisema ni lile la mwaka 1992 la kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini … "Tuliporejea mfumo wa vyama vingi hatukutunga katiba kwa kuwa haikuwa lazima. Unaondoa vile vifungu vinavyoondoa chama kimoja na vingine vinaendelea kama kawaida.

Kwa hiyo hata sasa hakuna haja ya kuandika Katiba Mpya, kitu chochote kinachotakiwa kingeweza kuingizwa katika Katiba iliyopo.

Mchakato wa Katiba

Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea nchini, mwanasiasa huyo ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo za ukatibu wa Bunge, Katibu Mkuu wa CCM na Makamu Mwenyekiti wa CCM, alisema tofauti zinazojitokeza nchini wakati huu zina sababu.

"Kwa wengine, mchakato wa Katiba Mpya umekuwa ni ajenda yao. Kwa mfano, Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010 walishaweka wazi kuwa wangeandika katiba mpya ndani ya siku 100 wakiwa madarakani. Wanaamini Rais Kikwete kakwapua ajenda yao, hivyo hawakufurahishwa kuona ajenda hiyo imechukuliwa na kutekelezwa na CCM.

"Hii ndiyo sababu ya misimamo mikali, ikiwamo ile inayojitokeza kwa sasa kwenye Bunge Maalumu la Katiba," alisema.

"Ni vyema mjadala uachwe uendelee kwa masilahi ya wananchi, kwanza unawafanya Watanzania wajue maana ya Katiba.

Ni sahihi waachwe wajadili Katiba wanayoitaka, kwani wengi wameweza kuelewa kuwa inahusu maisha yao, zamani nani aliijua?" alihoji.

Mfumo wa Serikali

Akizungumzia mfumo upi wa Serikali unaofaa Tanzania kutokana na mijadala inayokinzana kwenye Bunge Maalumu la Katiba, Msekwa alisema hana chaguo wala hajali iwapo ni Serikali mbili, tatu au moja.

"Sina choice (chaguo) wala sijali kwa sababu uimara wa Muungano unatokana na utashi wa kisiasa wa viongozi wakuu wa nchi, wala si idadi ya Serikali," alisema.

Katika suala la utashi wa kisiasa, Msekwa alisema umekosekana kwa pande zote mbili za Muungano, jambo ambalo linahatarisha uhai wake.

"Kwa upande wa Zanzibar, utashi wa kisiasa umekosekana, ipo mifano ya kauli kama za Maalim Seif Shariff Hamad anayesema hadharani kwamba tunahitaji Muungano wa mkataba.

"Kukosekana huku kwa utashi wa kisiasa nchini kunaweza kuvunja Muungano," alisema na kuongeza kuwa ndani ya CCM pia wapo ambao hawana utashi huo.

"Kwa mfano, kuibuka kwa kundi la wabunge 55, maarufu G55 ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1993 ni matokeo ya ukosefu wa utashi huo wa kisiasa.

"Hasira zao (wabunge hao wa G55) ziliamshwa na uamuzi wa Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya OIC," alisema Msekwa na kuongeza kuwa walihisi kuwa ungezuka mgogoro mkubwa wa kikatiba nchini ndipo wao wakaibuka na hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika.

Chanzo;Mwananchi
 
Hoja ya Mzee Msekwa inautata mkubwa na inaashiria changamoto kubwa ya kupata Katiba inayofaa kwa nchi yetu. Umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya unaeleweka na kila mtu na ndiyo maana watu walijitokeza kwa wingi kushiriki kutoa maoni nakadhalika. Yaelekea kwa kuwa rasimu iliyotolewa haiwapendezi wengi walio kwenye madaraka aidha uwezekano wa kufanya marekebisho makubwa sana unaonekana mgumu, kwa hivyo pole pole hoja inaanza kujengwa ya kuwa hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya. Kwa maana nyingine inafanana na ule usemi "kwa kuwa sisi hutukupata basi hakuna atakaepata" Hii kwa kweli ni aibu na fedheha kubwa. Ingefaa wote wanaohusika wakatafakari na kukubali kuangalia maslahi ya nchi kwa miaka mingi ijayo na tuache ubinafsi.
 
Waafrika ni wabinafsi sana. Yaani yeye keshapata anaona wengine hawastahili kupata. Maana kiukweli, kwa mfumo wa kikatiba uliopo, ni kwamba mtoto wa maskini ataendelea kuwa maskini milele, mfumo umejaa kulindana na kuogopana. Wanaolindwa ni Magamba na wanaoogopwa ni magamba ambao jeshi, polisi magereza mahakama vyote vyao. Vyote hivyo vinafanya kazi dhidi ya wanyonge na maskini. Katiba mpya walao imeshaonesha mwanga kidogo, lakini kwa sababu wanyonge hawana haki mijitu kina msekwa na wenzake wanafanya juu chini kuhujumu hatua muhimu ya kumuinua mwananchi mtanzania.

Ee Mungu tuepushe katika vishawishi, tusije watenda hawa wazee kitu mbaya...
 
hata mimi naunga mkono wa kutoandika katiba mpya bora hizo hela ingetumika kuboresha huduma za maji elimu afya na kilimo
 
Na bado alitowa maoni yake kwa tume ya warioba? mbona hakuyasema haya? Au ndio kaoteshwa leo?

1-8.jpg
 
Huyu mzee kigeu geu. Hana tofauti na H Mwakyembe. Ukitumikia CCM ni sawa unatumikia shetani maana inabidi ufuate usicho amini na ukane unachoamini.
 
Ingekuwa Kenya sijui kama huyu mzee angerudi nyumbani kwake salama bila kupata bakora mbili tatu -- yaani watu wameshatumia karibia billion 300 then mtu unakuja na kauli ya kejeli namna hii kweli?

Watanzania tuwe makini mno na wazee wa namna hii!! wanaweza kuhatarisha amani ya nchi yetu wakati wowote.
 
Huyu mzee kigeu geu. Hana tofauti na H Mwakyembe. Ukitumikia CCM ni sawa unatumikia shetani maana inabidi ufuate usicho amini na ukane unachoamini.
Tunaweza kuyadharau haya mawazo kwa sasa lakini kama alivyosema Mh. Komba juu ya kuingia msituni, ni wazi wasimamizi wa machafuko kwa jina la kulinda amani wapo wengi. Vijana kuuweni macho.

 
huyu mzee ameshafaidi pesa nyingi kutoka kwenye serikali ya ccm haoni umuhimu wa katiba mpya mbona hakusema mapema amesubiri mpaka wameshatumia karibu billioni 200 ndo anaibuka huu ni unafiki mkubwa
 
huyu mzee ameshafaidi pesa nyingi kutoka kwenye serikali ya ccm haoni umuhimu wa katiba mpya mbona hakusema mapema amesubiri mpaka wameshatumia karibu billioni 200 ndo anaibuka huu ni unafiki mkubwa

wewe taja kitu maalum ambacho katiba itanufaisha taifa.ukweli ni kuwa katiba ni mradi wa watu katika harakati za kisiasa majukwaani.mtanzania hanufaiki chochote.hili suala lifutiliwe mbali tuendelee na mambo ya maana.hata hii habari ya vitambulisho vipya vya kura ni ulaji tu.tukamilishe vitambulisho vya kitaifa na vitumike hata kwenye uchaguzi
 
hata mimi naunga mkono wa kutoandika katiba mpya bora hizo hela ingetumika kuboresha huduma za maji elimu afya na kilimo

Kwa heshima kabisa namuomba mwenye nchi asitishe hili zoezi la katiba mpya.hiki ni kichaka cha kutuchanganya na kuharibu fedha za serekali.hakuna manufaa yeyote kwa nchi.
 
Back
Top Bottom