Msc Chemical Engineering na Msc Engineering Management, ipi bora?

mzee mzalendo

Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
65
Reaction score
28
Poleni na majukumu ya kujenga taifa,

Kijana wenu nataka kurudi shule pale mlimani, nimewaza na kuwazua, nimeona niwashirikishe katika hili. Ipi kozi nzuri ya kuenenda katika hizo mbili ili kuweza kushiriki katika uchumi wa viwanda. Kwa sasa mimi ni PE Engineer

Tanzania kwanza

Nawasilisha

Kijana mzalendo
Changoko-SAME
 
Wewe unataka kufanyia nini baada ya kumaliza masomo?
Nataka hapo baadae, labda baada ya miaka minne au mitano nifanye shughuli zangu binafsi. Chemical eng ni kwa ajili ya environmental consulting firm, na Management ni kwa ajili ya enginnering projects. Je ipi ni bora zaidi kwa uchumi wa viwanda
 
Ushaur WANGU;
Achana na kusomea sifa, hiyo elimu ulonayo inatosha kabisa kupambana na changamoto za maisha.

Elimu ya nchi hii kwa sasa haina thamani kama zamani

DILI nyingi,
consulting films huwa wanaitegemea serikali.

Sasa
Tenda ZOTE sahv serikalini, wanapeana wao kwa wao taasisi za serikali.

Mpaka sasa Consulting film nyingi za private hazina kazi, nyingine zimefungwa.

Wakandarasi private hawana kazi& wengine wamefilisika hawajalipwa malipo yao.
DILI zote za ujenzi sasa wanapewa TBA.

Kwa sasa,
Tafuta mtaji, Fanya ujasiliamali

Kama huna mtaji, tafuta ajira kwa hiyo elimu ulonayo ili upate kianzio/ mtaji.

Kisha wekeza katika ujasiliamali.

Tambua kua, kwa sasa kua na
ELIMU KUBWA BILA KUA NA PESA MFUKONI, NI UPUUZ WA KIWANGO CHA LAMI

#### Nawasilisha####
 
Sio kwamba sina kazi, nina kazi ambayo kipato chake sio kibaya. Nipo kwenye ajira huu mwaka wa sita, na pia ni mkulima na mjasiriamali. Nina 32yrs, nataka nijipange kwa hilo, ila ushauri wako nimeuelewa kuwa fursa nyingi kwa sasa hazipo, ila mimi najipanga ili nishiriki vizuri kwenye uchumi wa viwanda. Nishauri katika hizo mbili
 
Kujiajiri
Mkuu nakushauri usome hyo MBA ambayo ukimaliza utakua tayari una knowledge ya Accounting, Marketing, Human resources, IT, Administration, Sales etc ambazo zitakusaidia katika mfumo mzima wa Entreprenueurship, yani utakua fully equipped na knowledge za kusimamia miradi yako.
 
sio mazuri sana Lakin kuna wakati comments za wadau zina chekesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…