'Msauzi' akiri kukutwa na bangi, afungwa miaka 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Msauzi' akiri kukutwa na bangi, afungwa miaka 3

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  RAIA wa Afrika Kusini, Hilton Miles (28) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela ama kulipa faini ya Sh 200,000 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa ya kulevya.

  Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Niku Mwakatobe baada ya mshitakiwa huyo kukiri kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mwakatobe amesema, mahakama inamtia hatiani mshitakiwa licha ya kujitetea kuwa ni kosa la kwanza na gari alilokutwa nalo hutumiwa na watumishi wengi lakini bado ni kosa la jinai kukutwa na dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria.

  “Kutokana na kosa hilo, nakuhukumu kulipa faini ya Sh 200,000 fedha za kitanzania ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa wengine,” amesema Hakimu Mwakatobe.

  Akijitetea, Miles kupitia kwa wakili wake Constatine Mutalewa, alidai dawa hizo za kulevya zilikutwa kwenye gari ambalo limekuwa likitumiwa na watumishi mbalimbali katika ofisi yao na kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza, anaomba Mahakama imuonee huruma.

  Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Hemedi Halidi kuwa mshitakiwa huyo ambaye ni Meneja Mradi wa mgodi wa Buzwagi Kahama, alikamatwa Juni 5, mwaka huu katika hoteli ya Tilapia, jijini Mwanza akiwa na dawa hizo.

  Alidai alikutwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika gari lake lenye namba za usajili T848 AFM aina ya Land Cruiser.

  Hadi tunakwenda mitamboni jana wakili wa mshitakiwa alikuwa akijiandaa kulipa faini ili mteja wake aachiwe huru.
   
Loading...