Msata Bagamoyo

Kikombe1

Senior Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
132
Reaction score
99
Nimepita barabara hii nikitokea Arusha. Kwa kweli ni safi na haina stress kama za ubungo. Wengine piteni mjionee
 
inavutia ukiwa Msata, lakn mwishoni ni majanga
 
Kuna kilometer 8 tu za mwisho ambazo ujenzi unaendelea....Ila majanga yake sio kama ya foleni za malori na daladala pale mbezi mwisho kuelekea ubungo hasa wakati wa jioni.
 
.ni road nzuri ukitembea ikiwa umtembeaji .ni nzuri ya kujiachia, isipokuwa Kati hapo kuna matuta ya kukera...
 
.ni road nzuri ukitembea ikiwa umtembeaji .ni nzuri ya kujiachia, isipokuwa Kati hapo kuna matuta ya kukera...
Barabara nyingi zimekua na karaha ya kusafiri maana matuta yamekua kama tupo shambani, kwani wameshindwa kubuni njia za watembea kwa miguu chini ya barabara( pedestrian bridge) badala ya kutumia matuta au hatuna wahandisi wa kuplani kabala ya ujenzi wa barabara?
 
ungetuwekea picha.wengine tuko huku Ntwara tutapita lin Msata


[h=2]Wednesday, May 29, 2013[/h] [h=3]Mkeka wa barabara ya Bagamoyo - Msata unakaribia kufika Bagamoyo[/h]
​
Ni Barabara yenye urefu wa Kilomita zipatazo 64 yenye kuunganisha Mji wa Bagamoyo na njia kuu ya Chalinze - Segera. Barabara hii imekuwa chini ya matengenezo na hali ilivyo sasa inaridhisha kwani ni takriban kilometa 15 zimebakia ili lami iweze kufika Bagamoyo. Kamera ya TembeaTz ilipita mitaa hii tarehe 26 Mei na kushuhudia hatua kubwa waliyopiga wakandarasi hao. Kwa wale wazoefu wa barabara hii, Mkandarasi yupo karibu kabisa na kile kijiji (maarufu kwa kuuza Nyanya na Vitunguu) baada ya kuvuka daraja la Mto Ruvu.


​
Kwa mujibu wa mwenyeji niliyeongozana nae, hivi sasa wasafiri wengi wa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro na Arusha) wamekuwa wakiitumia hii barabara kukwepa foleni na usumbufu wa unaotokana na ujenzi wa barabara ya Morogoro maeneo ya Kimara. licha ya usumbufu wa foleni, Barabara hii inaelzwa ya kuwa inampunguzia msafiri takriban kilometa zipatazo 60 kwenye safari yake kama angeendelea kwenda Chalinze, Kibaha mpaka Ubungo.


​
Ikikamilika kabisa, ni dhahiri wasafiri wengi wa mikoa ya kaskazini watakuwa wakiitumia​

​
Kwa sisi tunaopenda mambo ya pori, basi milango ya hifadhi ya Taifa ya Saadani itakuwa imefunguliwa. Kwa kutumia njia hii, mgeni wa hifadhi ya Saadani anaweza kufika kwenye hifadhi kirahisi. Wale wanaotoa visingizio vya umbali sasa waanze kuandaa kisingizio kingine. Ni matumaini yangu pia TANAPA na wadau wengine wa utalii wanafuatilia kwa karibu ujenzi wa barabara hii na fursa ambayo itaileta kwenye hifadhi ya Saadani.


 
Ni juhudi nzuri zinazofanywa na serikali yetu tukufu kuhakikisha kwamba mikoa yote inaunganishwa na barabara za lami.Pongezi sana kwa wizara husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…