Msanii wa filamu, Wastara kurejea nchini wiki hii

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
wastara45.jpg


Baada ya kuwepo kwenye matibabu takribani wiki tatu zilizopita nchini India, hatimaye msanii wa filamu, Wastara Juma anatarajia kurejea nchini wiki hii.

Habari kutoka kwa ndugu wa karibu wa msanii huyo ambaye yupo naye nchini India, zimesema wanatarajia kurejea nchini siku ya Alhamisi, Machi Mosi.

Amesema tayari operesheni ya mgongo imefanyika vizuri na atapewa dawa za kuendelea nazo kwa miezi sita akiwa hapa nchini.

Aidha, kwa upande wa mguu amepewa tiba na kuelekezwa masharti ya kufuata ili tatizo alilokuwa nalo lisimrudie na pia atakuwa akiendelea na dawa.

Wastara alifanikiwa kwenda kwenye matibabu hayo, Februari 3, mwaka huu baada ya kupata michango kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Rais John Magufuli aliyemchangia Sh15 milioni.

Kilichosababisha hadi afikie hatua ya kuchangiwa ni kutokana na Januari 4, mwaka huu, msanii huyo aliyekuwa mke wa Juma Sajuki (sasa marehemu), alijilipua mitandaoni kwa kuandika ujumbe kuomba msaada wa Sh37 milioni ili aende kutibiwa baada ya kuhangaika kuzisaka bila ya mafanikio.

Aliandika: “Mimi Wastara Juma mwigizaji wa filamu Tanzania naandika ujumbe huu mfupi sina budi, sina jinsi nahitajika kurudi hospitali India tokea (tarehe) 12/02/2017 ambapo nilitakiwa nifanyiwe matibabu kwa muda wa miaka miwili chini ya uangalizi wa hospitali.”

Chanzo: Mwananchi
 
Hamna mgonjwa hapo..
Akishuka Airport aeleze ilikuwaje cannula badala ya kupeleka damu kwenye mwili yake ilikuwa inapeleka damu kwenye kucha.
 
Huyu ndio kasababisha nimeijua cannula inakaaje kaz yake nin asant wastara
 
Back
Top Bottom