si halali hata kidogo..kama sekretarieti ya chama chini ya makamba imeishiwa mbinu ...iondoke...ni aibu!!
Mkuu ninakubaliana na wewe kabisa, majuzi nilimuuuliza mkuu mmoja wa CCM kwamba inawezekanaje kumpa Komba, shillingi millioni 50, kwa ajili ya uchaguzi mmoja tu tena wa Tunduru, na hizo hela zinaweza kuwa zimetoka wapi? na how did Makamba survive the ax majuzi Dodoma, kwa sababu sio siri kuwa uwezo wake ni mdogo kama kiongozi wa chama kinachotawala, amejiingiza sana kwenye majungu kati ya viongozi wa CCM, I mean aliyomfanyia Kigoda kwenye uchaguzi wa NEC, ilikuwa ni aibu nzito sana,
Mkuu huyu wa CCM, kutoka Visiwani, ambaye pia jana Jumamosi nilizungumza naye tena, akitaka more info kuhusu BOT,na hasa Balali, aliniambia kuwa CCM wanakutakana next month, this time watakutania Butiama, na kwamba itakuwa kiama kwenye hicho kikao, kwa sababu sasa hivi kuna vijana wengi wapya, ambao ndio hasa waliomuangusha Kingunge kwenye cc, na pia wakamkatalia Muungwana, kuwapitisha Msuya na Salim, kuingia bure cc, akasema kuwa na hii ishu ya BOT ndio kabisa utawaka moto, pia aliniahidi kujaribu kuigusa ishu ya Komba, ambayo alisema kuwa viongozi wengi wa juu, hawapendi kuigusa kabisa hiyo ishu!