Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 45
Msanii Mapunda aitosa CCM
na Agnes Mlundachuma
MSANII wa muziki wa Kiafrika, Fullgency Mapunda 'Mwana Cotide' ameamua kujitoa katika bendi ya Tanzania One Theatre inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na kujivua uanachama wa chama hicho baada ya kushindwa kumtekelezea mahitaji yake kulingana na makubaliano.
Mwana Cotide, ambaye awali alikuwa akifanya sanaa binafsi na pia uhamasishaji katika shughuli mbalimbali za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amefikia uamuzi huo baada ya kutolipwa mshahara wake kwa miezi mitatu kwa madai ya kuchunguzwa kwa madai kuwa ni mpinzani.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, iliyopatikana jana jijini Dar es Salaam, na nakala yake kusambazwa kwa Katibu Mkuu wa CCM na Mkurugenzi wa TOT Plus, Kapteni John Komba, anaeleza kuwa alijiunga na CCM, Agosti 28, mwaka jana kwa sharti la ujira mnono na kukabidhiwa kadi namba AB 1621644 na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, wakati huo, Kapteni Jaka Mwambi.
Mwana Cotide alisema Oktoba 6 mwaka jana, aliajiriwa na TOT akiwa kama msanii msaidizi chini ya Kapteni Komba, kwa barua yenye kumbukumbu namba CCM/PT36 155/5 akiwa na ngazi ya mshahara wa CMWK2M ambao ni sh 310,000.
Msanii huyo aliongeza kuwa, lakini hajawahi kulipwa mshahara tangu kipindi hicho, hivyo kuamua kubwaga manyanga.
"Ninajitoa CCM kwa kuwa msingi wa mimi kujiunga na chama hicho ulikuwa ni ajira na si sera wala itikadi, kwa kuwa wamekiuka makubaliano yetu nimeamua kujitoa rasmi, sharti letu lilikuwa ajira nono na huo ndio ukweli ambao Sekretarieti ya CCM inautambua," alisema.
Aliongeza kuwa, kutokana na sababu hizo na nyingine nyingi ambazo atazieleza baadaye anajitoa katika chama hicho.