Msamaha katika mapenzi ni ishara ya upendo wa kweli

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,109
9,407
Natumai mpo njema wakuu.

Msamaha katika mapenzi ni ishara ya upendo wa kweli, ukiona mwenza wako anaomba msamaha after kukosea ujue anayajutia makosa yake hivo anaomba samahani kusawazisha alipokosa.

Mtu anaekupenda kwa dhati ni rahisi sana kuomba samahani akikosea bt kama hana upendo wa dhati hata akukosee haoni umuhimu wa kuomba samahani, ukiona hivo ujue mnasogeza siku tu wala hamna upendo wa kweli.

Wakuu hii ni njia nyepesi sana ya kumjua mwenza ulie nae kama ni mtu sahih au lah.

Nawatakia pumziko jema.
 
Msamaha ndio upendo mkuu ukiona mmekoseana mkasameheana na maisha yakaendelea vzr basi jua upendo unaishi ndani yenu.

Kutofautiana kupo sana kwenye mahusiano na msamaha ndio humaliza tofauti zenu bila kusahau kujishusha kidogo kuupa msamaha nafasi ya kutenda kazi yake .
 
umefafanua vizuri zaidi.
 
Ni kweli msamaha wa kweli unasaidia kurudisha situation to normal, ila kuna watu wanajua kupretend kuomba msamaha(hamaanishi), yaani ni kama anafanya kwa kujilazimisha hivi na huku akirudia makosa yale yale.

Tusameheane na makosa yasirudiwe rudiwe
 
ukiwa na mtu anaomba samahan then anarudia kosa lile lile ujue kwako anasogeza siku, mtu anaemaanisha harudii kosa lile bt hukosea kwa mambo mengine coz binadam si mkamilifu.
 
Back
Top Bottom