Msaliti hahitaji Msamaha nyie CHADEMA

Msaliti hahitaji Msamaha nyie CHADEMA

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
7,005
Reaction score
9,264
Watuuuuuuuuuu ni Nguvuuuuuuuuuu

Habari za Kazi Wanajukwaa , Poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki kipindi hiki cha serikali ya Mama Samia,Kiukweli KAZI IENDELEE mpaka 2030

Miaka 6 iliyopota ya machozi na damu kwa upande wa CHADEMA tuliona wengi wakifungwa, wakisingiziwa kesi, wakijeruhiwa na hata kupotezwa na kuuwawa, hakuna chama cha upinzani kilichovuja jasho na damu kama CHADEMA, hakuna chama kilichopingwa n ahata kusemwa kinatumiwa na mabeberu kama CHADEMA, CHADEMA iliumizwa vibaya sana na naamini makovu yale hayawezi kufutika mapema.

Wapo walioachwa na vilema vya kudumu, wapo waliopoteza ndugu (baba, mama, watoto, mjomba, shangazi n.k),

Kuna watu/viongozi walikua CHADEMA wakaondoka kwa mbwembwe nyingi wakaondoka kwa kejeli na matusi wakisema CHADEMA imekosa dira, wakaondoka wakitukana mwenyekiti na viongozi wengine wengi wakiamini kabisa watadumu milele huko waendako wakisahau “today’s mine and tomorrow is never promised”

Wengine wakafika mbali sana wakikubaliana na wanayotendewa watu wa CHADEMA wakisema wamezidi ukanjanja

Lahaulaaaa……yakatokea

Leo hii naona wanataka kurudi kundini, naona CHADEMA inawapokea tu, inawatangaza (INADHANI SIFA SIJUI)

Mwingine Juzi amerudi anasema, “Hajarudi na V8 amerudi na pengo” sasa tumsaidiaje sisi, juzi wa Serengeti nae anaomba kurudi, yule si ndio aliondoka kwa kejeli na watakuja wengi sana kwasababu wenye chama chao waliokipigania kwa mjasho na damu wamerudi (baba zao hawakulala, hawakula, walikesha wakipigania chama chao)

Haiwezekani wao watake raha tu wasitake shida

CHADEMA hata Yesu mwenyewe alisema Ingekua heri msaliti asingezaliwa.
 
Chadema hawawezi kuwakataa wale wanaotaka kujiunga kwenye chama chao, sheria ya vyama vya siasa inakataza hilo, labda wasiwape uongozi.
 
Nelson Mandela alisamehe kila mtu hususani wale maandui wake wa kisiasa walio mfunga miaka 27, ila hakuweza kumsamehe mke wake Winnie Mandele, Msaliti hasamehewi, inauma sanaaa.... Chadema achana na hao wasaliti mtaua chama.
 
Kuna watu/viongozi walikua CHADEMA wakaondoka kwa mbwembwe nyingi wakaondoka kwa kejeli na matusi wakisema CHADEMA imekosa dira, wakaondoka wakitukana mwenyekiti na viongozi wengine wengi wakiamini kabisa watadumu milele huko waendako wakisahau “today’s mine and tomorrow is never promised”
kuna ushahidi usioacha shaka kwamba walikuwa na option mbili tu, Kuhamia CCM kuunga juhudi kwa ujira ama Kugoma then chamoto wakipate wao na familia zao.

Hawa ni LAZIMA wasamehewe maana ilikuwa wafanye hivyo kunusuru maisha yao na wapendwa wao.
 
Nelson Mandela alisamehe kila mtu hususani wale maandui wake wa kisiasa walio mfunga miaka 27, ila hakuweza kumsamehe mke wake Winnie Mandele, Msaliti hasamehewi, inauma sanaaa.... Chadema achana na hao wasaliti mtaua chama.
Acha kupotosha ukweli wewe, unajuaje Mandela(rip)hakumsamehe Nomzamo!let's facts hapa,Winnie aliendelea kuwa Mandela (surname)na siku ya msiba alikua mmoja wa wajane!
 
Kile kipindi cha kuunga juhudi kiliandaliwa kijuha sana.bahati mbaya nikwamba waliohama kwa mbwembwe hawakujua kua lolote linaweza kutokea wakati wowote.

Kwahiyo kama kuna aliyehama kwakufikiri anamkomoa mtu ajue alijidanganya kwasababu kwa chadema uko mbele kuna nuru zaidi kuliko upande alikokimbilia.

Kwahiyo kama kuna atakayejitokeza na kuomba samahani ni sawa tu akasamehewa ila kwa utaratibu sahihi utakaowekwa na chama.

Ninaamini chadema hadi hapa ilipofika haiwezi tena kubabaishwa na mamluki yoyote atakayejifanya anataka kuharibu chama.
 
Yule Mollel aliyesema kwamba Chadema ndio waliotaka kumuua Tundu Lissu aje aeleze vizuri.
 
Watakua wanaiiga ccm lowasa,sumaye ,msingida yule nawengine wengi walirudi ccm

Chadema kuwapokea hao nikujipalia Moto mkubwa sana
 
Watakua wanaiiga ccm lowasa,sumaye ,msingida yule nawengine wengi walirudi ccm

Chadema kuwapokea hao nikujipalia Moto mkubwa sana

Kurudi nyumbani sioni kama ni tatizo, lakini nafasi ya uongozi hapana.
 
kuna ushahidi usioacha shaka kwamba walikuwa na option mbili tu, Kuhamia CCM kuunga juhudi kwa ujira ama Kugoma then chamoto wakipate wao na familia zao.

Hawa ni LAZIMA wasamehewe maana ilikuwa wafanye hivyo kunusuru maisha yao na wapendwa wao.
Wengine tamaa tuu. Hawa akina lusinde Nani aliwaambia watakipata chamoto? Ni tamaa tuu
 
Back
Top Bottom