Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili wa kudumu vyama vifuatavyo

Mtazamo wangu wa kijinga ni kwamba kufuta usajili wa vyama hivyo alivyofuta Jaji Mtungi lengo lake ni kutaka kukifuta CUF. Kwa sasa hawezi kuanzia chama hicho maana kutazuka gumzo na kelele ya kufa mtu. Kwa kufuta vyama hivi tayari amepata reference ya kwamba "mbona vyama fulani vilifutwa kwa kukosa sifa za kuwa chama cha siasa na maisha yakaendelea" .

Sasa baada ya hili la kufuta vyama hivi kufaulu bila vurugu kutokea, hatua inayofuata nikuendeleza na kukuza plan B ya mgogoro ndani ya CUF. Hatimaye mgogoro huo utazusha hoja za chama ku-qualify kuwa disqualified. Ninahisi hoja kubwa zaweza kuwa ama vurugu zainazoweza kusababisha mauaji au kuwa connected na shughuli za kigaidi.

CUF - Hapa naona mnayokazi ya kufanya.
1. Jiepushe na mivutano ya nguvu ya misuri "physical confrontation"
2. Jiepushe na matamshi hatarishi kwa amani ya nchi.
3. Lile tamko la kutohubri siasa misikitini huenda nalo linafanyiwa kazi ili hatimaye litumike.
4. Any other reason to be fabricated or created by the body intending to DELET the Party!

Hivi na huu ni uchochezi kweli? La hasha, haya ni maoni.
 
Kile cha DOVUTWA kinatimiza masharti ya usajili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…