Msajili wa vyama vya siasa futa hiki chama cha CUF

Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,697
3,263
Wana jamvi,

Ningependa kutoa ushauri wangu na hasa kuhusiana na hiki chama ambacho inavyoonekana kimepoteza thamani sasa ya kuitwa chama cha siasa.

Kinachonishangaza zaidi inaonekana sheria haiko wazi hasa kuhusiana na nani ni nani kwa sababu haiwezekana kama sheria ya vyama na kulingana na msimamo wa Msajili wa vyama inamtambua bwana Prof. Lipumba halafu watu wengine pembeni kundi la Maalim Seif linaendeleza harakati zake kama kawaida.

Nini msimamo sasa wa sheria naona mnatuweka njia panda na kwa uzembe huu sasa watu wanamwaga damu. Nani awajibike. Nadhan kuanzia sasa tumtafute mchawi wa tatizo hili. Nani msimamizi wa sheria za hivi vyama na je hatua gani zinachukuliwa kwa wanaondesha harakati za kihaini ndani ya chama.

TUPEWE MAELEZO.
 
Wakat ye ndo mvurugaji mkuu wa mambo. Inabd waelewe WaTz wa leo sio wa mwaka 90. Figusi figisu zao na fitna tunaziona na tunazielewa,na ipo cku yatafika mwisho haya. kama msajili angekua kweli na nia ya kusuluhisha huu mgogoro tangu mwanzo wakat wanagombaniana vyeo angetafuta njia nyingine ya kusuluhisha sio kumrudishia uenyekiti prof lipumba ambae aliuacha kwa hiari yake mwaka 2015. Atleast angeitisha uchaguzi mpya angeonekana reasonable, sio kubariki chama kuwa na wenyeviti wawili. (Mmoja wa kumteua yeye, mmoja wa kuteuliwa na kamati kuu) NONSENSE!
 
kufutwa kwa CUF ni hasara kwetu sisi CCM waache wagombane hivohivo,kikifutwa hiki chama wanachama wote watahamia CHADEMA itakuwa shida kwetu CCM
 
Wana jamvi.
Ningependa kutoa ushauri wangu na hasa kuhusiana na hiki chama ambacho inavyoonekana kimepoteza thamani sasa ya kuitwa chama cha siasa. Kinachonishangaza zaidi inaonekana sheria haiko wazi hasa kuhusiana na nani ni nani kwa sababu haiwezekana kama sheria ya vyama na kulingana na msimamo wa Msajili wa vyama inamtambua bwana Prof Lipumba halafu watu wengine pembeni kundi la Maalim Seif linaendeleza harakati zake kama kawaida. Nini msimamo sasa wa sheria naona mnatuweka njia panda na kwa uzembe huu sasa watu wanamwaga damu. Nani awajibike. Nadhan kuanzia sasa tumtafute mchawi wa tatizo hili. Nani msimamizi wa sheria za hivi vyama na je hatua gani zinachukuliwa kwa wanaondesha harakati za kihaini ndani ya chama. TUPEWE MAELEZO.

chama kinachotakiwa kufutwa ni ccm. kosa namba moja ni cha kigaidi kinatumia magaidi kufanya fujo kwenye wapinzani wao.
mfano wa leo hawa ni magaidi wa lipumba kwa ufadhili wa ccm
 
Msajili wa vyama na Lipumba wanatakiwa kumtibu na kutoa huduma zote kwa huyo kijana alievunjwa mguu, kwa sababu wote wawili ndio chanzo cha matatizo yote yanayojitokeza.
 
Hilo ni wazo lako lakini ungefikiria kwanza kuna athari gani baada ya chama hicho kufutwa?

Kama tunavyojua, Mbunge ili awe bungeni lazima awe mwanachama wa Chama fulani cha Kisiasa. Maana yake, CUF ikifutwa itatulazimisha tuwafute wabunge wote wa CUF na uchaguzi kufanyika upya.

Kwa hiyo nchi tuingie kwenye hasara kubwa ya kupoteza mamilioni kwa sababu ya muingiliano tu wa maslahi baina Viongozi?

Kinachohitajika ni Msajili kuacha kuingilia majukumu yasiyomhusu na kupendelea upande fulani kwa manufaa ya Chama kingine.
 
Ndo naanza kujua nia ya hawa jamaa wanaotuma watu kufanya vurugu!Kumbe mnafanya uchokozi ili mpate sababu?!!Kwa nini msipeleke mswada tu bungeni wa kufuta vyama vyote kuliko mikakati hii watu waumie wateseke wengine wapotee kwa akili ya kusapoti vyama vya upinzani?
 
Na mrajisi afute ndoa ya baba yako na mama yako. Kwa sababu mama yako kamweendea kinyume baba yako!
 
Back
Top Bottom