PreGE2025 Msajili wa Vyama vya Siasa fanya kazi yako, unapwaya sana halafu sijui kama unaona au makusudi?

PreGE2025 Msajili wa Vyama vya Siasa fanya kazi yako, unapwaya sana halafu sijui kama unaona au makusudi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
477
Reaction score
1,017
Msajili wa vyama vya siasa punguza unazi kidogo alafu fanya kazi yako. Kuna mahali unapwaya na kushindwa kuficha hisia zako.

Juzi umemsikia mwenezi wa CCM alichosema hadharani mbele ya wananchi. Hakusema chochote, hujatoa onyo lolote kwa CCM kama msajili wa vyama, hujawaita CCM waje kutoa maelezo kutokana na tuhuma nzito alizotupia chadema na kampeni yao ya no reform no election.

Unajua wazi alichosema Makala ni nonsense na kwa mamlaka yako, utashi wako na majukumu yako kimsingi ulitakiwa kumwita Makala na CCM yake watoe ufanunuzi juu ya tuhuma hizo ambazo kimsingi Zina athari kwa nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kiutawala pia.

Haya yote hujayafanya ila Cha ajabu umemsikia Mchome, kada aliyefukuzwa chadema akisema eti no reform no election imepitishwa na viongozi wachache tena akimaanisha kuwa kauli mbiu hii eti imeanzishwa juzi kati na viongozi wapya bila kushirikiana wajumbe wote na wewe bila kufikiria eti umewaita kujieleza, are you serious? Mbona Makala na kauli zake za kuligawa taifa hujazishughulukia?

Kwa hiyo upo tayari kuona CCM ikiharibu nchi? Upo kwa maslahi ya CCM? wewe ni msajili wa CCM au vyama vyote vya SIASA?

Hatuna Imani na msajili wa vyama vya siasa, ni pro CCM na haendani na mahitaji na mazingira halisi ya siasa za Tanzania kwa mwaka 2025.

Wakati wa Chadema kumtangaza Makala kuwa ni mtu wa hivyo na huyu Msajili wa vyama vya siasa ajumuishwe huko, wote wawili wadharauliwe na kupuuzwa vikali

Pia soma

 
Ingekuwa ni nchi nyingine, hadi sasa ungekuwa na wachangiaji wa hoja wasiopungua laki moja.
 
Back
Top Bottom