Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amemrudishia uanachama aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Leticia Mosore na kumruhusu kuendelea na wadhifa wake katika chama hicho.
Barua iliyosainiwa na ofisi ya Msajili inasema Leticia hakupewa nafasi ya kuitwa na kusililizwa ili kujibu tuhuma zinazomkabili kam inavyoelekeza kwenye ibara ya 10(4) ya Katiba ya NCCR Mageuzi.
Leticia alivuliwa nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti na kufukuzwa uanachama wa chama hicho kwa sababu ya kuhujumu UKAWA kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na kupanga njama za kumdhuru mwenyekiti wa NCCR Taifa Mhe.James Mbatia.
Tuhuma hizo ziliwasilishwa na Mwenyekiti wa Makamishna wa chama hicho taifa, Peter Mushenyela ambaye awali alishirikishwa na Leticia kuihujumu UKAWA. Mushenyela alielezwa na Leticia kuwa amepewa fedha na CCM ili kumchafua Lowassa. Na alitakiwa atafute viongozi wenzie kadhaa ambao kila mmoja aliahidiwa Shikingi Milioni 10 ili watoe tamko la kumchafua Lowassa kwa niaba ya NCCR Mageuzi.
Katika kutekeleza mpango huo Leticia alimtumia Mushenyela ticket ya ndege ya kutoka Bukoba (nyumbani kwake) kuja Dar na kumlipia hoteli ya kifahari ambayo alikaa kwa siku 10 akipanga mipango na Leticia ya kuhujumu UKAWA. Pia walipanga kumdhuru Mhe.Mbatia kwa kwa kumteka, kumjeruhi na kumtengenezea picha chafu ambazo wangezisambaza mitandaoni.
Baada ya Mushenyela kukusanya ushahidi wote ikiwemo rekodi ya sauti ya Leticia, aliwasiliana na Mbatia na kumueleza mipango yote miovu iliyopangwa na Leticia. Hslmashauri kuu ya NCCR ilikaa Julai 16, mwaka jana, kujadili suala hilo na kwa kauli moja wakaridhia kumvua Leticia uongozi wa Chama hicho na kumfukuza uanachama.
Leticia aliandika barua kwa Msajili wa vyama kulalamilia maamuzi hayo, akidai kwamba hakuitwa kuhojiwa, na hakupewa nafasi ya kusikilizwa. Hatimaye Msajili amemrudishia uanachama na nafasi yake Umakamu mwenyekiti. Barua ya Msajili inasema ofisi yake inamtambua Leticia kama Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi.
Kufuatia kukingiwa kifua na Msajili, Leticia ameliambia gazeti la HabariLeo (la tar.03/04/2017) kwamba anatarajia kuwasili ofisini kwake leo kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake ya kiofisi kama Makamu Mwenyekiti, kwa lengo la kuendelea kukijenga chama hicho.
[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG];
Ofisi ya Msajili iache kukandamiza demokrasia nchini. Jaji Mutungi hatendi haki hata kidogo kwa vyama vya upinzani. Hii si mara ya kwanza kumrudisha ofisini mtu aliyefukuzwa au kujiuzulu kwenye chama cha siasa. Prof.Lipumba alijiuzulu kwa hiari yake na baraza la uongozi la chama hicho likaridhia maamuzi yake, lakini from nowhere Ofisi ya Msajili ikamrudisha madarakani. Huyu Leticia nae alifukuzwa baada ya tuhuma nzito dhidi yake leo nae karudishwa madarakani. Inakera sana.
Hivi mtu anayedaiwa kupanga njama za kumteka na kumjeruhi Mwenyekiti wake unawezaje kumrudisha aendelee kufanya kazi na Mwenyekiti huyohuyo? Hivi mtu anayedaiwa kupanga njama za kuhujumu UKAWA unamrudishaje NCCR ambayo ni member wa UKAWA?
Halafu hoja ya kumrudisha iliyotolewa haina mashiko kabisa. Kwamba hakusikilizwa. What a weak argument. Atasikilizwaje wakati inadaiwa aliitwa kwenye kikao akakataa kwenda? Sasa mtu aliyeitwa akakataa alitegemea asililizweje? Afuatwe nyumbani?
Jaji Mutungi ni Mwanasheria mbobevu. Anafahamu kitu kinaitwa "Default Judgement" katika sheria. Yani kufanya maamuzi kwa kusikiliza upande mmoja (wa mlalamikaji) kwa sababu upande wa utetezi umekataa au umeshindwa kuwasilisha utetezi (Judgment rendered because of the defendant's failure to answer or appear). Kwa mantiki hiyo Jaji Mutungi alitaka Leticia ahojiwe vp wakati alikataa wito wa Halmashauri kuu? Doesn't he know the principle of Default Judgement?
Na kama hoja ni kusikilizwa mbona hajamrudisha madarakani Sophia Simba? Maana nae alifukuzwa uanachama na kuvuliwa uongozi bila kusikilizwa. Au principle ya kusikilizwa ina apply kwa wapinzani tu, sio CCM??
Naona ofisi ya Msajili inatumika vibaya. Hii trend ya kurudisha watu waliofukuzwa/kujiuzulu inaweza kuleta mtafaruku mkubwa wa kisiasa nchini. Tusipokemea hili tusije kushangaa hata yule "daktari" aliyekimbilia ughaibuni na mchumba wake, akarudishwa kwenye nafasi yake siku moja. We must say NO now.!
Malisa GJ