Msajili wa Vyama atoa neno baada ya Maalim Seif kufungua ofisi mpya

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,296
Baada ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Maalim Seif, kufungua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa Kata ya Mzimuni, Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Msajili wa Vyama vya Siasa amesema anaamini chama hicho kinafanya mambo yake kwa kuzingatia sheria.
upload_2017-6-7_9-10-35.jpeg

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi,amezungumza na gazeti la Habarileo, ambapo alisema hajapata taarifa yoyote ya chama hicho, kufungua ofisi mpya zaidi ya kuona katika vyombo vya habari.


“Ukiondoa taarifa za kwenye media sijapata taarifa yoyote kutoka CUF labda wawe wameleta leo (jana), lakini naamini chochote wanachofanya wanaelewa taratibu wataleta taarifa,”alisema Jaji Mutungi.


Jaji Mutungi alisema sheria inawataka wanapofungua ofisi watoe taarifa ndani ya siku 14, ambazo hazijaisha hivyo anaamini wanajua hilo. Upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad wamefungua ofisi hizo, baada ya tukio la kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Buguruni na kundi la Profesa Ibrahim Lipumba.


Jaji Mutungi alisema atakapopokea taarifa rasmi ataangalia kama taratibu zikifuatwa kwani ufunguaji wa ofisi mpya una taratibu zake. “Nikiletewa taarifa ndio nitajua kama walifata taratibu au la, ufunguaji wa ofisi una taratibu zake najua wanazijua pia,” alisema Jaji Mutungi.


Chanzo: Habari Leo
 
Vipi hajatia neno kuhusu Mwenyekiti wa ACT kukimbia majukumu yake kwa ajili ajira mpya? Ingekuwa ni Chadema angeshatoa onyo la kukifuta hadi muda huu simply hakijatimiza takwa la kisheria la chama kuwa na Mwenyekiti. Nchi hii ni vituko.
 
kazi ipo kufungua ofisi mpya lazima msajili wa vyama ajue,mbona ccm wanafungua ofisi zao bila vikwazo?lini hawa wateule wataelewa kuwa nchi hii belong to all of us?,halafu tatizo la chairperson wa opposition party kuwa RC halioni,nimehuzunika mno hivi karibuni kumwona mzee Tindwa eti naye akitiliwa umuhimu wa LESOTHO kuwa na uchaguzi wa haki wakati hakuzingatia hilo wakati wake.
 
Back
Top Bottom