Msaidizi wa raisi masuala ya lishe ni mgonjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidizi wa raisi masuala ya lishe ni mgonjwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maluluma, Jul 29, 2012.

 1. m

  maluluma Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HABARI kuhusu uteuzi wa dkt. Wilbard Lorry aliyeteuliwa kuwa mshauri wa Rais masuala ya lishe kama ilivyo tolewa kupitia mtandao wa jamii forum tarehe 19/7/2012 ni PROPAGANDA zinazofanywa na baadhi ya watu. Ndio maana hiyo habari haikuwa na ufafanuzi wowote kuhgusu huo ugonjwa alionao licha ya kuwekwa picha ya ya dkt. lorry. Kimsingi hapa lishe pana majungu mengi sana na msingi wa majungu haya ni makundi yaliyokuweka wakatui wa utawala wa bwana ndossin mkurugenzi mkuu mtendaji aliye ng'olewa mwezi machi 2012. Hivyo, habari hii kwa vyovyote vile imeandikwa na wapambe wa ndossi.

  Kihistoria bwana lorry amewahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe tanzania. Wakati wa kipindi chake mahusiano baina ya wafanyakazi yalikuwa mazuri na hata yeye lorry binafsi alisaidia wafanyakazi pale alipoweza kufanya hivyo. Hakukuwa na makundi na alijitahidi kuwa jirani na wafanyakazi kwa kiasi kikubwa. Kama kulikuwa na dosari basi zilikuwa ni kwa kiasi kidogo. Lorry aliondolewa mwaka 2002 na kikundi ambacho lengo lake lilikuwa ni kuchukua madaraka ya taasisi kwa kutumia mbinu chafu na kufanikiwa kumwondoa. Kwa muda wote huo lorry alikaa kimya hakutaka kujihusisha na malumbano yoyote ktk taasisi.

  Utawala wa ndoss ulipoingia madarakani na wapambe wake, tukashuhudia taasisi ikaanza kuporomoka kwa kasi ya ajabu. upendeleo ukawa juu watu wachache wakawa wananeemeka ktk taasisi, mikutano ya taasissi vurugu tupu, maamuzi yakawa mikononi mwa mtu mmoja, mishahara kuchakachuliwa na kuchelewa sana, madeni ,kupanda vyeo kwa sura badala ya vigezo, mishahara kupangiwa kwa sura, undugu, ukabila na upendeleo wa aiina nyingine. Ndio maana hata alivyoondolewa machi mwezi taasisi ililipuka kwa shangwe kana kwamba wafanyakazi wametolewa gerezani, vuvuzela zilipigwa, sherehe zilisherekewa. Hii haikuwafurahishwa wapambe wa bwana Ndossi.

  Tangu aondolewe na taasisi kushikwa na kaimu mkurugenzi bwana Jeje kwa miezi mitatu inaonyesha mabadiliko kuelekea hali yake ya awali. madeni ya wafanyakazi kwa kiasi kikubwa yanalipwa, wafanyakazi wanafuraha na taasisi yao hata walioacha kazi wanapenda kurudi na kutembelea, usafiri uliositishwa na ndossi umerudishwa na mikutano inaendeshwa kwa utulivu mkubwa na wafanyakazi kuridhika na majibu ya menejimenti tofauti na jeuri iliyokuwa ikifanywa wakati wa ndossi. Kwa ujumla haki ya mfanyakazi inazingatiwa licha ya ukata uliopo.

  Kwa ujumla taarifa ktk jamii forums ni kuweweseka kwa watu ambao waliona kuwa ubabe, unyanyasaji na kunyima haki za watu wengine ni furaha kwao na hata taasisi ibomoke wao walifurahi. Hivyo mabadiliko yaliyotokea ghafula kuanzia mwezi machi mwaka huu hawajaamini na kuyakubali na kwamba kwao watu wanapaswa kufurahia maisha badala ya wacghache au kikundi cha wachache. HII NI PAMOJA NA KUCHAGULIWA KWA DKT LORRY KUWA MWAKILISHI WA RAIS KTK MASUALA YA LISHE. HIVYO MABADILIKO YALIANZA YANAPASWA YAUNGWE MKONO NA WAPENDA MAENDELEO WOTE HAOPA TAASISI NA TANZANIA KWA UJUMLA. TUNAHITAJI SANA MABADILIOKO NA MAGEUZI KTK TAASISI HII.
   
Loading...