GE2025 Msaidizi wa mbunge mstaafu akamatwa na TAKUKURU Tarime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Elisha Samo ambaye ni Katibu wa Mbunge mstaafu wa Jimbo la Tarime Mjini, Mhe. Michael Mwita Kembaki, anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Tarime kwa tuhuma za kuendesha mikutano ya kisiasa kinyume na taratibu za Chama Cha Mapinduzi @ccmtanzania

Inadaiwa kuwa mikutano hiyo haikufuata mwongozo rasmi uliotolewa na Katibu Mkuu wa chama, hali inayotafsiriwa kama ukiukaji wa kanuni za chama na utovu wa nidhamu kwa mujibu wa taratibu za kisiasa ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa na Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Tarime, DBC. Hery Mchume, hatua ya kumkamata msaidizi huyo wa Mwita Kembaki ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusiana na tuhuma za kuwakusanya wajumbe wanaotarajiwa kupiga kura za maoni hapo kesho kwa ajili ya kuwagawia rushwa kuwashawishi kumpigia kura Michael Kembaki anayewania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini.

Akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV, Kamanda Mchume alithibitisha kuwa uchunguzi huo unalenga kubaini kiwango cha ukiukwaji wa taratibu pamoja na iwapo kulikuwa na matumizi mabaya ya nafasi ya kisiasa aliyonayo mhusika.
 
Hizi one-size-fits-all forums zinawanufaisha zaidi incumbents. Watiania wapya wanahitaji muda zaidi kuzunguka na kujitambulisha kwa wapigakura!
 
Back
Top Bottom