Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,802
- 1,606
Michango yetu ni msaada mkubwa!Habari zenu, Wiki kadhaa zilizopita nilirudi nyumbani kumkuta mume wangu na mjomba wake wakiwa wanazungumza.Nilitulia sehemu nikawasikiliza kiasi,nilichanganyikiwa.Nikaondoka, badae nikarudi nikajikausha kama hamna nilichosikia.Mume wangu alikuwa anamueleza mjomba wake mpango wa kuoa tena, na mjomba wake alikuwa akimsupport.Sisi wakristo,tulifunga ndoa ya kanisani.Mume wangu alisisitiza kuwa itabidi amuoe huyo mwanamke maana anampenda sana, na mwanamke amesema bila ndoa yeye anataka waachane,hawezi kukubali kuwa hawara.Nanukuu "Hata hivyo sijapata kukutana na mwanamke tukapendana naye kama yule".Maneno haya yanatoka kwenye kinywa cha mume wangu wa ndoa,na baba wa mtoto wangu.Kwa ufupi plan ilikuwa inapangwa namna ya kufanya hili jambo kwa utulivu na makini.Naomba ushauri, mana sijui pa kuanzia, kumbuka haya mambo alikuwa anayaongea na mjomba wake,na mjomba aliongea kama mtu anayemjua kabisa huyo mwanamke anayeongelewa.
i see Maria Roza ngoja kwanza nipate coffee ndo nirudi hapa pagumu mwenzio akinyolewa .......:coffee::coffee:
Dah!Kweli wanaume wengine ni hatari!Well kama amemsikia akiyasema hayo mwenyewe kilichobaki ni kujulishwa ili awe na uhakika!Kwanza ajiandae kupokea jibu lolote!Akusanye nguvu za kuweza kupokea na kukabilia na chochote kile atakachoambiwa!Ni ngumu ila kama mumewe kaamua kweli then amchukue mwanae wakatafute maisha yao mbele kwa mbele!Akimng'ang'ania mwanaume asiyempenda na anaeweza kua amemchoka ataishia kunyanyasika tu!Pole yake!
nadhani mumeo ni mtu makini,kama ataweza kukuletea mwenzio wa kukusaidia co mbaya,tena umesikia akisema anampenda sasa tatzo liko wapi? We tulia kama umesikia ni kusubiri utekelezaji.
Naungana na wewe kabisa ambassador, hebu apate muda wa kumuambia anachokijua then amsikie kwa mdomo wake anasemaje?Kama hamna ugomvi muombe mwende mahali patulivu mkishapiga stori zikakolea muulize kwa upole kama kweli anakupenda kwa dhati. Akisema anakupenda mwambie umepata taarifa za uhakika kwamba ana mpango wa kuoa. Atakurupuka kukuuliza nani kakwambia, mwambie unataka kusikia toka kwake. Hapo ndo pa kuanzia.......
Na akisema hakupendi muombe aweke wazi sababu za kutokupenda. Baadae mnaweza kuwashirikisha wazazi kadri ya ugumu wa issue. Pole
Lakini huyu mwanaume hajasema kuwa hampendi mke wake wa sasa! Japo nahisi walikuwa wana mtest huyu mke wa sasa maana walijua anatabia za kuchungulia na kunyatia mazungumzo!
UTAFANYA WATU WAJINYONGE :laugh:
Jamani huyo dada asikurupuke kuondoka, sikuhizi kuna siasa za maji taka, watu wanakuchanganyia unakimbia kwa mihasira yako, mwisho wa siku unagundua mchezo mambo yanakuw ndio basi tena. wanasema ukiona manyoya keshaliwa huyo.... aangalie sio kukimbiakimbia:roll:
Huyo anayetaka kuolewa hafahamu kama kuna mwenzake ndani ya ndoa? Anang'ang'ania kuingia nyumba ya mwenzake, afahamu mwenzake alipendwa kama yeye na iko siku naye atatafutiwa mwingine. Ndugu yangu penzi likishachuja kunakuwa hakuna tena raha ya kuishi pamoja, kama unaweza ondoka na mwanao mkaanze maisha na Mungu atakuwezesha kwa kila namna. Nimeweza.[/QUOTE]
Kwenye kolezo, hongera sana na pole pia.