Habari zenu wakuu wa JF
Sitaki kupoteza mda wenu kwa maneno marefu.
Nipo kwa kusudi Moja tu, Kumuombea kazi mwanamke jasiri ambaye kwa Sasa amepigwa na upepo wa maisha. Alikuwa amejitahidi kujitegemea, akajikusanyia mtaji mdogo na kuanzisha biashara yake ya kujikimu.
Kwa bahati mbaya vijana wahuni walimvamia usiku akiwa njiani kutoka kwenye biashara. Wakampora kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga na kumvunjia ndoto zake papo hapo, mtaji wake uliishia mikononi mwa wasio na huruma.
Leo hii hana pakuanzia tena, Si mvivu si mkaaji ni mchapakazi mwenye heshima, nidhamu na moyo wa kujituma lakini Sasa kila kitu kimeyumba kwake.
Anaishi Dar es salaam, mbagala kijichi, hivyo kama nafasi hipo karibu na eneo hilo hata kwa utaratibu unaowezekana tafadhari tuwazie namna ya kumuinua
Nakuja kwa unyenyekevu kuwaonba wale wenye uwezo wa kumpa kazi yoyote ya halali, anafanya kwa heshima na kujituma.
Anaweza kufanya kazi za usafi
Anaweza kumsaidia madukani au hotelini
Anaweza kuwa muhudumu au hata winga wa duka kubwa
Kazi yoyote ya halali isiyo ya udhalilishaji yenye malipo ya halali ambayo siyo ya unyonyaji atafanya kwa moyo wake wote
Kuhusu elimu yake amesoma hadi darasa la saba, lakini akili ya kazi na heshima ni daraja la juu
Tafadhari kama unayo nafasi inayoweza kumsaidia kurejea kwenye mstari wa matumaini nipe ujumbe, Nitakupatia mawasiliano yake kwa Nia njema tu, siyo kwa maswali ya kashfa na kejeli
Tusimcheke aliyeanguka maana kesho, sisi tunaweza kuwa mahali pake, msaada wako unaweza kuwa njia ya kusaidia waliowengi.
Asanteni sana, Mungu hawabariki kwa moyo wa huruma
Mwambie ajaribu hizi;
Anahitajika binti wa kazi maeneo ya Kijichi mbagala Dar es salaam.
Majukumu
1. Kupika chakula cha wote
2. Kufua na kupasi
3. Kufanya usafi wa ndani na nje ya nyumba/ bustani
Vigezo
1. Awe msafi sana
2. Awe na miaka kuanzia 18+ na kuendelea
3. Awe anatokea mikoa ya Dodoma, morogoro, Pwani
5. Awe na heshima
6. Awe mwaminifu
7. Awe amechangamka
8. Mwenye kujituma
9.awe mkristo
Mshahara .
Atalipwa kiasi Cha Tshs 60,000/= kwa mwezi
NB: familia ni ya watu watatu ,hakuna mtoto yeyote .
Kwa mwenye huhitaji wa hiyo fursa na mwenye hivyo vigezo apige simu kwa namba: 0711679445 anahitajika haraka🙏.
NAFASI YA KAZI
Natafuta mhasibu wa kike mwenye Diploma au Degree.
SIFA ZA MWAOMBAJI
1.Jinsia niya Kike na Awe na Umri usiozid miaka 28.
2.Ajue kutumia vizur program za kihasibilu especially Microsoft Excel.
Nb:Kituo cha kazi ni Mkoa wa Njombe.
Kampuni inajihusisha na kuuza vinywaji vya aina zote pia Boss ana magari amabayo yanajihusisha na usafirishaji wa Abiria na Mizigo.
*Mshahara ni kuanzia Sh 400,000/= kwa mwezi na pia mshahara utakuwa unaongezeka kulingana na utendaji kazi wako pia posho Boss kasema anatoa.
Pia Boss anamiliki Guest,Lodge n Bar
So muhasibu atakuwa na jukumu la kusimamia mapato na matumizi ya vyanzo vyote hivyo vya mapato.
Kwa aliye tayari na anasifa hizo hapa juu anichek Inbox Haraka ili aanze kazi hata kesho tu.
Inbox me your Cv through 0679301815...
Good morning Mr Robert, naomba ushare kwenye group nahitaji vijana wa marketing and sales kwa ajili ya interview immediately. Kampuni ni Bestan Textiles location banana Dar es salaam.
Contact. +255 716 444 938