mtoto ya simba
Member
- Jul 6, 2025
- 14
- 19
Habari zenu wakuu wa JF
Sitaki kupoteza mda wenu kwa maneno marefu.
Nipo kwa kusudi Moja tu, Kumuombea kazi mwanamke jasiri ambaye kwa Sasa amepigwa na upepo wa maisha. Alikuwa amejitahidi kujitegemea, akajikusanyia mtaji mdogo na kuanzisha biashara yake ya kujikimu.
Kwa bahati mbaya vijana wahuni walimvamia usiku akiwa njiani kutoka kwenye biashara. Wakampora kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga na kumvunjia ndoto zake papo hapo, mtaji wake uliishia mikononi mwa wasio na huruma.
Leo hii hana pakuanzia tena, Si mvivu si mkaaji ni mchapakazi mwenye heshima, nidhamu na moyo wa kujituma lakini Sasa kila kitu kimeyumba kwake.
Anaishi Dar es salaam, mbagala kijichi, hivyo kama nafasi hipo karibu na eneo hilo hata kwa utaratibu unaowezekana tafadhari tuwazie namna ya kumuinua
Nakuja kwa unyenyekevu kuwaonba wale wenye uwezo wa kumpa kazi yoyote ya halali, anafanya kwa heshima na kujituma.
Anaweza kufanya kazi za usafi
Anaweza kumsaidia madukani au hotelini
Anaweza kuwa muhudumu au hata winga wa duka kubwa
Kazi yoyote ya halali isiyo ya udhalilishaji yenye malipo ya halali ambayo siyo ya unyonyaji atafanya kwa moyo wake wote
Kuhusu elimu yake amesoma hadi darasa la saba, lakini akili ya kazi na heshima ni daraja la juu
Tafadhari kama unayo nafasi inayoweza kumsaidia kurejea kwenye mstari wa matumaini nipe ujumbe, Nitakupatia mawasiliano yake kwa Nia njema tu, siyo kwa maswali ya kashfa na kejeli
Tusimcheke aliyeanguka maana kesho, sisi tunaweza kuwa mahali pake, msaada wako unaweza kuwa njia ya kusaidia waliowengi.
Asanteni sana, Mungu hawabariki kwa moyo wa huruma