Msafiri. Oldies

Msafiri. Oldies

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,171
Reaction score
1,733
KISA CHA MSAFIRII
_____________________

Mwaka 2000 katika ukumbi wa Mambo Club (baadae ukaitwa Maisha Club) uliopo pale Oysterbay jijini Dar, lilifanyika tukio kubwa la kihistoria la muziki wa kizazi kipya nchini. Kundi la Hip Hop la Kwanza Unit lilikuwa likizindua albamu yake ya Tatu iitwayo "Kwanzanias". Uzinduzi ule ulikuwa na matukio makubwa mawili ya kihistoria.

Kwanza, albamu hiyo ilikuwa ndiyo albamu ya kwanza ya muziki wa kizazi kipya nchini kutoka kupitia CD badala ya Tape (Cassette), lakini pili, uzinduzi huo ulishuhudia Kwanza likiwa kundi la kwanza la Hip Hop kupanda stejini kuimba sambamba na Gwiji wa muziki wa dansi nchini, Marehemu King Kikii.

Uzinduzi ule ulituvutia wengi sana. Nakumbuka nilifika Mambo Club mapema sana na kulipa kiingilio cha Shilingi 2000 getini, kisha nikapewa CD ya albamu ya "Kwanzanias" bure mlangoni kama OFA. Albamu hii ninayo mpaka leo, na naendelea kuitunza sana kama ukumbusho wa tukio lile la kihistoria.

Albamu ya "Kwanzanias" ilikuwa na jumla ya track 24 ambapo track namba 7 kwenye mpangilio wa CD ya Albamu ile ulikuwa wimbo uitwao "Msafiri". Wimbo huu ndiyo uliopelekea King Kikii kuwepo stejini sambamba na Kwanza Unit usiku ule.

Wimbo wa "Msafiri" ulitungwa na kuimbwa mwanzoni mwa miaka ya themanini na bendi ya Ochestra Safari Sound (OSS) iliyokuwa ikitumia mtindo wa "Masantula" enzi hizo. King Kikii ndiye aliyekuwa mtunzi wa wimbo huo uliopata umaarufu mkubwa.

Wakiwa kwenye ubora wa hali ya juu, Kwanza Unit wakaurejea kuuimba upya wimbo huo katika mahadhi ya Rap na kuufanya kuwa moja ya tungo zao zilizopendwa na wengi. Msafiri ni kati ya nyimbo za Kwanza Unit zilizowatangaza sana na kuchochea hata wasiokuwa mashabiki wa Hip Hop kupanda kuusikiliza.

Wimbo huu unaelezea hali ya binadamu kutotakiwa kukata tamaa katika maisha pamoja na changamoto zote anazopitia, na hata Kwanza walipourejea kuuimba tena hawakutoka nje ya msingi kusudiwa wake, na kubaki mulemule kwenye misingi ya kile kilichozungumzwa na King Kikii miaka 20 iliyopita.

Pamoja na kundi hili kuwa na wasanii wengi, wimbo huu uliimbwa na Marapa wawili, Chief Rhymson (Zavara) na Robert Mwingira (D-Rob), huku Rapa KBC (Kibacha) akiimba kiitikio chake (Chorus) na kufanya kuwa moja ya track kali za muda wote za Kwanza Unit.

Baada ya track ya Msafiri kuchangia kuipa mafanikio makubwa albamu ya "Kwanzanias", Marapa wengi wa Kwanza Unit wakaripotiwa kusafiri kweli ughaibuni katika kujitafuta maisha bora zaidi na hivyo wimbo huo kuonekana kama umesababisha matokeo ya kile walichokiimba.

Shuka nao hapa chini ujikumbushe:

**************

Kiitikio: KBC
--------------------
Mimi Msafiri bado nipo njiani
Sijui lini nitafikaaaa..?
Naulizia watu kule ninakokwenda
Sijui lini nitafikaaaa

Verse 1: (Chief Rhymson):
-----------------------

Hii ndio Picha
Kabla ya Pazia la udongo
Ndani ya futi 6
Vita, kila watu 9 kati ya 10
Dhidi ya Hali duni
Naelekea njia ya Ughaibuni
Nimezungukwa na dhoruba
Nishapagawa
Sioni Rasi wala Ghuba

Ya Allah.!
Njaa, Chomoza
Shuhudia roho zinavyoangamia
Hali ya hewa imechafuka
Giza lauficha utakatifu
Kote sioni kitu
Mateso bila chuki
Mkushi bado hushtuki
Wapi, Yupi, Lini,
Si lazima uende shule
Jibu lake lipo mjini

Songa mbele, Songa
Huyawezi kaa chonjo
Saa mbaya mjomba
Pesa yaleta mvuto
Msukosuko,
Pamoja na Mabalaa
Yaliyozagaa
Nyuzi 360
Chief Rhymson Makini
Wala sichoki
Mwajiri wangu mi Passport
Ubongo Viza
Kweli yanalipa
Mapinduzi ya fikra

Usawa huu
Kufuatwa huko huko
Uliko juu
Nani ajaze hili Jedwari
Dash..dash...gani
Zinabuganywa bila tahadhari
Farasi Motokari
Punda au Ngamia
Yote bye, kama umeweka nia
We Mkwanzania.!

Verse 2: (D Rob)
------------------------

Nilianza na Mkwanza
Nilikuwa msema
Hadithi siisemi tena
Rob si Robby Tena
Maovu ndio yamejaa
Hakuna mema
Niite Zomba

Nataka kupiga bunda
Duniani ka motoni
Naota ndoto za peponi
Namuona Shetani
Aniuliza, we ni nani
Na unataka nini
Pesa magari
Na majumba ya kifahari
Njoo unifuate Mimi

Nakuwa Makini
Yo.! nakwenda kwa kasi
Lakini naona giza
We napiga yowe
Nasonga mbele
Litakalokuwa na liwe
Nipo mwenyewe katikati

Nyuma mbali mbele mbali
Nakutana na mambo mengi
Hili mradi tu hatari
Unyama hakuna Utu night kali
Ni dahari na hali hali, Sheli
Wakati hatuna kitu
Safari ni ndefu, Yo.!

Kama majeshi na mitutu
Wazungu na Makapu
Wazima na wafu
Eeh Mungu, walaze pema
Peponi Amina
Waliotuacha katika safari
Tutaonana tena
Kama nilivyosema mwisho
Tutarudi tena
Kwanza U.N.I.T.
King Kikii vipi, mbona hatufiki.?

(Rudia Kiitikio🙂

Verse 3: (Chief Rhymson)
-----------------------

Kafiri Ubatizwe Msafiri
Bila ya upeo wa Akili
Hauna Asili Utajiri
Kabla ya tafsiri, tathmini
Tafakari, tafadhali
Nini ujanja duniani
Zaidi ya kusoma

Ufikapo Roma
Fanya kama wafanyavyo Warumi
Himaya hii ni ya Kwanzania
Wote karibuni
Mgeni siku ya kwanza
Ya Pili mpe jembe akalime
Haya shime, haya shime
Vita hivi si vya rungu
Mkuki wala Sime

Nakana shtaka la Utoro
Safari ndio kwanza imeanza
Wazee wa Baraza, Mahakimu
Majaji na Wanajimu
Wanafalsafa
Wakufunzi na Walimu
Maprofesa ndani ya Elimu
Ya Saikolojia
Watawa ndani ya Parokia

Maandiko Makuu
Qur'an, Torati na Biblia
Fuata ukweli
Na fununu ya inapoishia
Hii Safari
Mabonde, Majabali na Milima,
Mi nafuata maji ya uzima
Tiba, Kitinda mimba
Hakika nitashinda

Vitu na thamani isiyo na kipimo
Dhahabu na Almasi
Enzi za mashimo ya Mfalme Suleiman
Yote yamebaki hadithi
Na huko nchi ya Misri
U-Mungu mtu
Ulishamshinda Firauni
Ole wako useme Rap Uhuni

Adili na nduguze
Waliobaki Makini
Fanya tathmini,
toka 90 Hadi wewe uingie mjini
Mimi bado nashika mpini.

0713 555 773

#Balozi.............✍️
 
Back
Top Bottom