Msafiri Kafiri

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Waungwana,
hii ni hali halisi ya barabara ya kuelekea lindi/mtwara
ni kipande cha km 64 tu lakini shughuli yake inaanzia masaa 2 hadi manne
 
Attachments

  • 100_0739.JPG
    100_0739.JPG
    861.1 KB · Views: 329
kwa kweli kile kipande cha barabara kinakera sana! nilipita mwaka 2009 Desemba nilikutana na watu wanaweka vipimo na wakadai baada ya miezi sita itakuwa imekamilika,lakini hadi leo hakuna chochote kero ni palepale!
 
Huyo mkandarasi nasikia ana godfather serikalini basi ni jeuri kwelikweli(M/S Kharafi and Sons)
 
Halafu unakuta mmekwama siku mbili hivi weee si mchezo balaa lake

wenyeji humo washajua mkikwama tu wanasogeza sufuria za mihogo ya kuchemsha kwa sh hamsini hamsini...mkiringa njaa ikibana fresh mnaigombea kwa mia mbili mbili...halafu choo machakani
 
hicho kipande kipomahali panaitwa somanga, nilipita early mwishoni mwa 2008, ni hicho ndo kilikuwa kisumbufu zaidi njia nzima. Walidai panakichanga sana na inabidi uchimbwe uondolewe wakalete kifusi kingine wamwage ndo ujenzi uanze! Lakini nnaona pamekua sugu.
 
nijuavyo mimi kazi za ujenzi barabara hutanguliwa na upembuzi yakinifu..je hawakuliona hilo?/
 
Usikute kuna madini hapo so jamaa anacheza hapo weeee akiyachukua ukijazinduka kwishneh madini yote. Uliza Chimwaga wachina hawakupenda maliza kujenga kisa ?????
 
Kazi ipo aisee wenzetu wanazidi vumbua tren za umeme sio tupo bado na barabara:shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth:
 
wenyeji humo washajua mkikwama tu wanasogeza sufuria za mihogo ya kuchemsha kwa sh hamsini hamsini...mkiringa njaa ikibana fresh mnaigombea kwa mia mbili mbili...halafu choo machakani
Ha ha ha... Mpaka mje kupata funguo zenu maji yameisha mwilini....
 
Tatizo la hii barabara wenyeji hawataki iishe, itaua biashara kabisa..... pamoja na pombe kutema cheche iishe baada ya miezi 6 lakini haitowezekana!!!
 
Hiyo inaitwa 'kasi zaidi, ari zaidi, nguvu zaidi' badala ya hilo li-monster machine la kujengea barabara lijenge barabara linafanya kazi ya kunasua magari - hivi hayo mafuta linalotumia kunasua mabasi na labda malori yanaingia kwenye gharama za ujenzi?
 
Namkumbuka Richard Mabala enzi zile anaandika makala zake gazeti la Majira alikuwa na heading moja inayosema "KUSINI TUSINI"
Kwa bahati ndiko ninakotoka, tumezoea na wala siyo kuwa hatupendi mahali hapo paishe na kupitika bali sisi siyo aggresive> kwa mara ya mwisho tulijaribu kutoa sauti na pale Mbuge wetu mmoja aliposema " basi tujiunge na Msumbiji" baada ya kuchoshwa na ahadi hewa.
 
mtwara na lindi ni karibu kuliko moshi na arusha lakini tab tup kufika wakati wa majira ya masika..
au tanroads hawajamlipa mkandarasi?
ngoja tuone pumzi za magufuli
 
Back
Top Bottom