Msafara wa Pinda waleta kero Arusha

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Msafara wa Pinda waleta kero Arusha

na Grace Macha, Moshi

MSAFARA wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi ulizua tafrani mjini hapa baada ya watu kukaidi amri ya kuegesha magari yao pembeni ili kuruhusu kiongozi huyo apite.

Hatua hiyo ilikuja baada ya waendesha magari na watumiaji wengine wa barabara kuu ya Moshi-Arusha kuamriwa kusimama kwa zaidi ya dakika 40 ili kupisha msafara wa waziri Mkuu aliyekuwa akitokea Arusha kwenda Moshi.
Wananchi hao waliokuwa kwenye magari ya abiria na ya binafsi walianza kusimamishwa kuanzia maeneo ya KIA , majira ya saa 10:10 asubuhi kwa magari yaliyokuwa yakitokea Moshi kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA ) na Mkoa wa Arusha.

Magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa pembeni mwa barabara kwenye maeneo mengine kama vile Bomang’ombe , Kwasadala, mferejini, Maili Sita, Karanga na kwenye Mzunguko wa barabara ya Arusha.

Hata hivyo, uvumilivu wa madereva wa magari yaliyokuwa yakielekea Moshi walikosa uvumilivu na wakaamua kuondoa magari baada ya kuona msafara huo haupiti, jambo lililowaacha vinywa wazi askari wa usalama barabarani na wale wa usalama wa taifa.

Katika hali ya kushangaza, magari yaliyoamua kukaidi amri hiyo, yaliendelea na safari hadi Moshi mjini bila kutokea kwa msafara wa Pinda kama ilivyokuwa imeelezwa na askari hao.

Baadhi ya madereva walilalamikia kitendo hicho huku wengine wakihoji sababu za polisi kuwasimamisha muda mrefu barabarani bila kuwa na uhakika wa taarifa wa eneo alipofika kiongozi huyo.

“Mimi nina wageni nawapeleka KIA lakini nimesimamishwa zaidi ya nusu saa na askari hawataki kutusikiliza sijui itakuwaje wageni hawa wakikosa lake litajwe gazetini.

Dereva mwingine ambaye aliyekuwa anaendesha gari la msafara uliokuwa ukielekea kwenye mazishi maeneo ya Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro alilalamikia kitendo hicho kwa madai kuwa watachelewa kuzika mwili wa marehemu ambao walikuwa nao kwenye gari.

Mmoja ya madereva hao, John Mushi alihoji sababu za polisi kuwasimamisha wakati kwa kawaida msafara wa viongozi hutanguliwa na gari inayosafisha njia (sweep car) ambayo ikipita magari yote hukaa pembeni kupisha msafara.
Msafara wa Waziri Mkuu aliyekuwa akienda mjini Moshi kufungua mkutano wa Jukwaa la Maendeleo la Mkoa wa Kilimanjaro (KDF) ulifika mjini Moshi majira ya saa 11:15 ambapo ulienda moja kwa moja Ikulu Ndogo kabla ya kuelekea eneo la mkutano Hoteli ya Kilimanjaro Cranes.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Yusuph Ilembo, alipoulizwa juu ya suala hilo alisita kutoa majibu badala yake alitaka atafutwe Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, ambaye alipopigiwa simu zake za kiganjani zilikuwa zikiita bila kupokewa.

Chanzo: Tanzania Daima Jumamosi 17 Desemba 2011.

Msafara wa Pinda waleta kero Arusha

na Grace Macha, Moshi

MSAFARA wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi ulizua tafrani mjini hapa baada ya watu kukaidi amri ya kuegesha magari yao pembeni ili kuruhusu kiongozi huyo apite.

Hatua hiyo ilikuja baada ya waendesha magari na watumiaji wengine wa barabara kuu ya Moshi-Arusha kuamriwa kusimama kwa zaidi ya dakika 40 ili kupisha msafara wa waziri Mkuu aliyekuwa akitokea Arusha kwenda Moshi.
Wananchi hao waliokuwa kwenye magari ya abiria na ya binafsi walianza kusimamishwa kuanzia maeneo ya KIA , majira ya saa 10:10 asubuhi kwa magari yaliyokuwa yakitokea Moshi kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA ) na Mkoa wa Arusha.

Magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa pembeni mwa barabara kwenye maeneo mengine kama vile Bomang'ombe , Kwasadala, mferejini, Maili Sita, Karanga na kwenye Mzunguko wa barabara ya Arusha.

Hata hivyo, uvumilivu wa madereva wa magari yaliyokuwa yakielekea Moshi walikosa uvumilivu na wakaamua kuondoa magari baada ya kuona msafara huo haupiti, jambo lililowaacha vinywa wazi askari wa usalama barabarani na wale wa usalama wa taifa.

Katika hali ya kushangaza, magari yaliyoamua kukaidi amri hiyo, yaliendelea na safari hadi Moshi mjini bila kutokea kwa msafara wa Pinda kama ilivyokuwa imeelezwa na askari hao.

Baadhi ya madereva walilalamikia kitendo hicho huku wengine wakihoji sababu za polisi kuwasimamisha muda mrefu barabarani bila kuwa na uhakika wa taarifa wa eneo alipofika kiongozi huyo.

"Mimi nina wageni nawapeleka KIA lakini nimesimamishwa zaidi ya nusu saa na askari hawataki kutusikiliza sijui itakuwaje wageni hawa wakikosa lake litajwe gazetini.

Dereva mwingine ambaye aliyekuwa anaendesha gari la msafara uliokuwa ukielekea kwenye mazishi maeneo ya Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro alilalamikia kitendo hicho kwa madai kuwa watachelewa kuzika mwili wa marehemu ambao walikuwa nao kwenye gari.

Mmoja ya madereva hao, John Mushi alihoji sababu za polisi kuwasimamisha wakati kwa kawaida msafara wa viongozi hutanguliwa na gari inayosafisha njia (sweep car) ambayo ikipita magari yote hukaa pembeni kupisha msafara.
Msafara wa Waziri Mkuu aliyekuwa akienda mjini Moshi kufungua mkutano wa Jukwaa la Maendeleo la Mkoa wa Kilimanjaro (KDF) ulifika mjini Moshi majira ya saa 11:15 ambapo ulienda moja kwa moja Ikulu Ndogo kabla ya kuelekea eneo la mkutano Hoteli ya Kilimanjaro Cranes.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Yusuph Ilembo, alipoulizwa juu ya suala hilo alisita kutoa majibu badala yake alitaka atafutwe Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, ambaye alipopigiwa simu zake za kiganjani zilikuwa zikiita bila kupokewa.

Chanzo: Tanzania Daima Jumamosi 17 Desemba 2011.

Ni muhimu suala hili likaanza kujadiliwa kwani wananchi tunateswa sana na misafara ya viongozi. Jijini Dar si raisi, makamu, waziri mkuu, mkuu wa polisi, wake wa raisi, waziri mkuu, makamu wao, akina seifu hamadi kila mtu anasababisha foleni kubwa barabarani. Ni lazima Watanzania tupinge kusimamishwa mara kwa mara na misafara ya viongozi kwani pale magari yanaposimamishwa mafuta mengi yanapotea bure, watu wanakosa miadi yao na shughuli nyingi za kimaendeleo zinasimama.
 
Tanzania bado tuna safari ndefu. Viongozi ambao hawana tija wanakwamisha kazi za maendeleo kwa njia ya misafara yao isiyo na tija.Mwisho wa siku hicho kidogo kitakachozalishwa na wananchi kiishie kulipa posho zao.
 
Ni muhimu suala hili likaanza kujadiliwa kwani wananchi tunateswa sana na misafara ya viongozi. Jijini Dar si raisi, makamu, waziri mkuu, mkuu wa polisi, wake wa raisi, waziri mkuu, makamu wao, akina seifu hamadi kila mtu anasababisha foleni kubwa barabarani. Ni lazima Watanzania tupinge kusimamishwa mara kwa mara na misafara ya viongozi kwani pale magari yanaposimamishwa mafuta mengi yanapotea bure, watu wanakosa miadi yao na shughuli nyingi za kimaendeleo zinasimama.

Mkuu hapo umeongea,me najionea kiongozi asie na makuu ni mzee Mwinyi akijitokea zake Mikocheni sometimes tunabanana nae Moroco mataa, hapa juzi kati bonge la foleni, kuchungulia dirishani eti makama wa pili wa raisi naloz seif
Safari bado ndefu
 
Huyu waziri wetu mkuu misafara yake imekuwa haina tija tena, badala yake imegeuka na kuwa kero na kizuizi cha maendeleo nchini.

Hivi majuzi, mwezi wa 11/2011 mwishoni, alitembelea maeneo ya viwanda Mwanza South mkoani Mwanza. Yaani ilikuwa kero tupu. Magari yamezuiliwa kwa zaidi ya dakika 45 kwenye barabara kuu kisa eti waziri mkuu anatembelea viwanda!! Sasa uzalishaji na shughuli nyingenezo za maendeleo zitafanyikaje iwapo kiongozi mmoja tu kati ya makumi wanaoongozwa kwa misafara anasimamisha shughuli zote kwa kisingizio cha protokali za usalama??!! Hawa miungu mtu wa karne hii wanakera sana ati!
 
Hivi tishio la Al Shabaab limeshaisha?

Kwa kweli Mkubwa wangu maana ni muhimu sana kwa hawa jamaa hasa wale wa ngazi ya juu mpk wanaofuata. Mwenye kujua Al-shaabab wanavyopatikana atujuze hasa wale wenye mabomu ya kujilipua. Maana hawa mafisadi ndiyo dawa yao tu!
 
Back
Top Bottom