Msafara wa Dkt. Magufuli wapata ajali Dodoma

Msafara wa Dkt. Magufuli wapata ajali Dodoma

Quantum

Member
Joined
Oct 28, 2013
Posts
53
Reaction score
21
Msafara wa Dkt.Magufuli umepataja ajali Dodoma ukitokea Manyoni baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kuingia Manyoni Mjini (Manyoni Access Road) yenye urefu wa kilomita 4.8. Ajali hiyo ilihusisha gari la Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi na la Meneja wa Wakala wa Barabara Dododma.Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ukiachilia Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi ni pamoja na Msajili wa CRB Eng. Boniface Muhegi, Mwenyekiti wa bodi ya CRB Eng.Consolatha Ngimbi na Meneja wa Wakala wa Barabara Dodoma Eng.Chimagu na mtu mwingine mmoja, hata hivyo majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Hata hivyo Dkt.Magufuli hakujeruhiwa kwenye msafara wake.



Ilivyokuwa: Dkt.Magufuli baada ya kuweka jiwe la msingi Manyoni, aliongozana na msafara wake akilekea Dodoma Mjini amabako alitakiwa kuhutubia na kufungua Taa za Barabarani Mjini Dodoma. Bahata mbaya msafara wake ukapata ajali. Hata hivyo Dkt.Magufuli aliweza kuendelea na ziara Mkoani Dodoma ambapo alihudhulia na kufanya ufunguzi wa Mataa ya barabarani mjini Dodoma akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mkuu wa Wilaya, Wanajeshi pamoja na wananchi.



Uwekaji Jiwe la Msingi Barabara ya kuingia Manyoni Mjini: Dkt.Magufuli aliweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kuingia Manyoni Mjini (Manyoni Access Road) yenye urefu wa kilomita 4.8. Baadhi ya viongozi waliohudhrulia uwekaji wa jiwe la msingi ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh.John Zefania Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba Mashariki ndugu Mgana Izumbe Msindaiwa, Wenyeviti wa Bodi, wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara na wananchi.

Picha za Matukio:

9015139fdfac96537650796b9374f36f.jpg fecc670813efe1dcfc8faa3d4f32f692.jpg 66254e700569c9e0df725c178530cc79-1.jpg

Matukio ya Ajali ya gari la Mtendaji Mkuu wa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi, ambapo watu watano walijeruhiwa.


f8b762129671ddb8002b82927566e625.jpg
Ufunguzi wa Mataa ya barabarani mjini Dodom,Dk.Magufuli,Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mkuu wa Wilaya, Wanajeshi pamoja na wananchi.
e81dc1aebca48d540eda9578c6a914b4.jpg
Mataa ya Barabarani Mjini Dodoma, walioketi ni timu nzima ya ufunguzi ikiongozwa na Dkt.Magufuli
668d8cee42db4657cfd8cf520207a68f.jpg
Uwekaji wa jiwe la Msingi barabara ya kwenda Manyoni Mjini, picha ya kumbukumbuku Dkt.Magufuli,Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mh.John Zefania Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba Mashariki ndugu Mgana Izumbe Msindaiwa, Wenyeviti wa Bodi, wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara na wananchi.
cbe227a913efeaa04411e2d0350f26e7.jpg
Uzinduzi wa Barabar ya Kwenda Manyoni Mjini.

4725df31660203edbb55e091adc6d2ae.jpg
Dkt.Magufuli akikata utepe uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kuingia Manyoni Mjini wengine ni Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh.John Zefania Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilaya, Mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba Mashariki ndugu Mgana Izumbe Msindaiwa, Wenyeviti wa Bodi, wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara.

 
Duuuu gari imearibika vibaya,poleni sana majeruhi.
 
Mbona mawaziri na Marais wa Kenya sijawahi pata kusikia wamefungua taa za barabran au barababra, hospital, shule na vitu vyengine vilivyolazima kwa maendeleo ya watu kwa shwangwe kama ilivyo Tz!
 
Mungu awaponye haraka kwa huruma yake.
 
Huo msafara ulikusanya wataalamu wengi na magari mengi bila sababu za msingi,

Poleni majeruhi!!!!
 
Mbona mawaziri na Marais
wa Kenya sijawahi pata kusikia wamefungua taa za barabran au barababra,
hospital, shule na vitu vyengine vilivyolazima kwa maendeleo ya watu
kwa shwangwe kama ilivyo Tz!

ukichunguza kwa makini utakuta gharama za ziara ziko juu ya gharama za mradi.

Only in Tanzaniaccmjk
 
Thamani ya hayo magari ni madarasa mangapi shule za msingi, ni zahanati ngapi. Yangenunuliwa magari ya bei nafuu.
 
Mbwembwe zote hizo ni 4.8 km. Jamani wabongo wakati mwingine let's pretend to be serious🙁
 
Mbona mawaziri na Marais
wa Kenya sijawahi pata kusikia wamefungua taa za barabran au barababra,
hospital, shule na vitu vyengine vilivyolazima kwa maendeleo ya watu
kwa shwangwe kama ilivyo Tz!

kila kinachotokea kenya unakifahamu?
 
Magufuli kazi kutembea na wandishi wa habari taa za kuongozea barabarani nazo mpka uzinduzi?

Km4.8 unaweka jiwe ka msing?

Shame on u gambaz.!
 
Mbona mawaziri na Marais wa Kenya sijawahi pata kusikia wamefungua taa za barabran au barababra, hospital, shule na vitu vyengine vilivyolazima kwa maendeleo ya watu kwa shwangwe kama ilivyo Tz!

Mkuu hujui Tanzania ni nchi ya majanga...
Anyways poleni magamba kwa kufikwa na majanga.
 
Pole sana majeruhi

Bungeni walituambia kuwa magari yenye zaidi ya miaka nane yanasabisha ajali sana. Please magufuli afuate sheria ya magari chakavu kuepusha ajali hizi.
Poleni wajeruhiwa na tutii sheria za nchi bila shuruti.
 
Magufuli kazi kutembea na wandishi wa habari taa za kuongozea barabarani nazo mpka uzinduzi?

Km4.8 unaweka jiwe ka msing?

Shame on u gambaz.!

Hawana kazi za kufanya zaidi ya utalii wa ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom