Kuna mashine ya kufulia aina ya Indesit wixl 143s. Ilipata tatizo la drain pump kuungua pamoja triac husika. Nimepata spare husika na kuziweka. Mashine inafua lakini bado pump haizunguki ikifikia kuondoa maji. Nimejaribu kuunganisha pump direct nje kwenye umeme inafanya kazi. Nimecheki nyaya zinazoleta umeme kwenye pump kwa kutumia tester na bulb ya kawaida zinawasha inapofikia drain/kutoa maji. Nashindwa nianzie wapi. Nawakaribisha wataalam mlioko humu