Msaada wenu wana jamii, kilimo cha mpunga

Bushman_king

New Member
Sep 27, 2019
1
0
Habari za majukumu , naombeni msaada wa mawazo nahitaji kuingia kwenye kilimo cha mpunga naomba anae jua mchanganuo wa haya

1.Gharama za kukodi shamba kwa ekari 1
2.Kulima,palizi kwa ekari 1
3.Mbegu kiasi gani kwa ekari 1

Mazingira ya kilimo naombeni kujua kwa mikoa ya Morogoro au Mbeya.
 
Morogoro maeneo mengi kukodi shamba si chini ya laki moja, kulima ekari moja na kupandikiza week laki 2!! Palizi weka elfu 60. Mbegu debe moja
 
Habari za majukumu , naombeni msaada wa mawazo naitaji kuingia kwenye kilimo cha mpunga naomba anae juachanganuo wa hays
1.ghalama za kukodi shamba kwa ekari 1
2.kulima,palizi kwa ekari 1
3.mbegu kiasi gani kwa ekari 1

Mazingira ya kilimo naombeni kujua kwa mikoa ya morogoro au mbeya
Majukumu yako poa, bila shaka na kwako pia.
Kulingana na hoja yako, ninapenda kuchangia baadhi ya mambo niyajuayo juu ya kilimo hiki cha mpunga. Mimi ni mkulima wa zao hili ktk mkoa wa Songwe wilaya ya Momba bonde la Kamsamba.
SIFA ZA BONDE HILI
~Ardhi yenye rutuba
~Uhakika wa maji
~Mavuno mengi
~Mpunga unaotoa mchele mzuri na wenye soko kubwa, ni mchele namba 1 kwa soko la mikoa ya nyanda za juu kusini.
~Gharama za wastani ktk uendeshaji
~Matumizi ya mbolea si ya lazima
~Miundombinu ya barabara iko vizuri
~Rasilimali watu inapatikana
~Shamba la 200000 unaweza panda na kuvuna mara2 kwa msimu

GHARAMA/EKA1
✓Kukodi shamba 100000-200000
✓Kukatua/kulima(ng'ombe) 40000
✓Kusawazisha/kuvuruga 40000
✓Mbegu plastik mbili 20000
✓Kitalu cha mbegu 10000
✓Kung'oa mbegu 25000
✓Kupanda 70000-100000
✓Kung'olea/palizi 25000-40000
✓Kufyeka 50000
✓Kusomba 25000
✓Kupiga 50000
Hizi ndizo hatua muhimu za kuzingatiwa ktk kilimo cha mpunga.

RATIBA YA MSIMU
>Kusafisha shamba disemba mwanzoni
>Kulima Disemba mwishoni, januari au februari mwanzoni.
>Kuvuruga na kupanda wiki moja au zaidi baada ya kulima
>Palizi/kung'olea wiki 3 na kuendelea baada ya kupanda.
>Kuvuna mwezi April hadi Mei.

Kama kuna swali au mchango wowote wa ziada unakaribishwa.
 
✓Kupiga 50000... Ahi nimependa Sanaa hii kitu hivi heka 1 waweza toa roba ngapi kiongozi pia kama huto jali nahitaji msaada wa Hali na Mali juu yakupata detail Zaidi za kuhusu hapo +255756889283
Hizi ndizo hatua muhimu za kuzingatiwa ktk kilimo cha mpunga.

RATIBA YA MSIMU
>Kusafisha shamba disemba mwanzoni
>Kulima Disemba mwishoni, januari au februari mwanzoni.
>Kuvuruga na kupanda wiki moja au zaidi baada ya kulima
>Palizi/kung'olea wiki 3 na kuendelea baada ya kupanda.
>Kuvuna mwezi April hadi Mei.

Kama kuna swali au mchango wowote wa ziada unakaribishwa.
 
Kiongozi nimevutiwa Sanaa nahii kitu samahani nahitaji msaada wako Kwa Hali na Mali wakupata taarifa Zaidi za hapo kama huto jali kiongozi 255756889283
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom