Msaada wenu wa haraka, wembamba unaninyima amani

Msaada wenu wa haraka, wembamba unaninyima amani

faru joni

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
478
Reaction score
734
Habarini za muda huu, poleni na miangaiko ya hapa na pale kuakikisha tunapata chakula cha siku kwa familia na binafsi
.
.
Niende kwenye point moja kwa moja:
.
.
.
Mimi ni kijana umri wangu ni range (25--30), mpaka sasa nimeshapitia mahusino na mabinti watatu, nina urefu wa kutosha (sio kama hashim thabiti no), ila tatizo linakuja kwenye umbile la mwili wangu nimekuwa na changamoto kadha wa kadha
.
.
Kwenye familia yangu baba yangu Ana mwili wa kutosha na amepanda ewani vizuri sana, mama yangu hana mwili wa kutosha ni mwembamba
.
.
Binti wa kwanza, aliniacha kwa kuwa alipenda sana ninenepe na niwe na nyama nyama za kutosha ila haikuwa ivyo nilidumu nae kwa mwaka mmoja akaniacha
.
.
Binti wa pili, uyu alinishauri sana nile vizuri ninenepe, ila haikuwa ivyo tukaachana (kwa sababu nyingine tofauti na wembaba ingawaje alikuwa akinisisitiza sana ninenepe)
.
.
Uyu wa tatu nilimpenda mno tena mno ametoka kuniacha Nina week ya nne sasa (mwezi mmoj), uyu alinishauri Nile mayai, uji wa ulezi na maziwa..kwa mazingira nilikuwepo sikuweza kubalance ivyo chakula kwa sababu,
.
.
Nilichaguliwa kusoma chuo kikuu cha dodoma, collage of informatics, course ya computer engineering
.
.
Nilikutana na masomo magumu mno na changamoto ya chuo (collage ya informatics )ilikuwa ikinipa pressure muda wote
.
.
Kulingana na changamoto za chuo sikujali kuhusu wembaba wangu tena

Baada ya uyu binti wa tatu kuona bado nipo vilevile akaamua kunitafutia sababu na kuachana na mimi (ila Nina uhakika wa asilimia 95.5%) nimeachwa kwa ajili ya huu wembaba
.
.
Nimemaliza chuo mwaka huu, na matokeo yametoka poa nasubili graduu tu, sina tena streess nipo happy kabisa!!

Naombeni msaada wenu ni njia zipi nizifate angalu nipate mwili-mwili, sitaki kuwa kibonge sana ila napenda kuwa na nyama za wastani

Naombeni maoni yetu

Asante na mungu awabariki
 
Mimi pia mwembamba mkuu, changamoto pekee binafsi nakutana nazo,watu wananisihi niache kufanya mazoez..eti kutokana na huu wembamba ntakufa.

Maana nina tendency ya kuamka daily sa kumi na moja kasoro alfajir...tangu nkiwa chuo hata baada ya kuanza kazi
 
inamaana humu jf kila member amesoma mpaka chuo?

Wacheni ulimbukeni wa kutaja vyuo tu pasi na ulazima
 
Acha kuhangaika mkuu....dawa ni moja tuu ...kula mdudu daily mida ya jion jion plus bia ...nakuhakikishia ndani ya mwezi mmoja utaona mabadiliko makubwa sana mkuuu....mimi nilikula mpaka sasa nahangaika jinsi ya kukipunguza kitambi mkuu
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Back
Top Bottom