Vaa kiatu cha mhusika,tusiwe wepesi wa kutoa majibu mepesi kwenye hoja ngumu,mwenzio naomba msaada wa kimawazo ili aweze kutatua changamoto zake.
"""""""""'""'''""""""""""""""""
Kwako mtoa maada kutokana na uzoefu nilionao mimi,naomba nikushauri kuwa kuna njia nyingi sana za kufikia mafanikio yako,lakini pia sio lazima njia tulizojipangia zitimie ndo tufikie malengo yetu,naweza kukushauri kuwa hebu kama unaona inafaa tulia kwa mwaka mmoja ujipange kwani kwa hoja yako eti utatumia pesa ya kujikimu kulipa karo hapo ni kujidanganya maana pesa ya kijikimu ni 1.9+M kwa mwaka na huwa haiji kwa mkupuo ,kiasi hiki ni kidogo sana,na ukilazimisha utatumia nguvu nyingi lakini mwisho wa siku yaweza kuwa usifikie malengo yako.
Hivyo nikusuhi kwa laki moja uliyonayo hebu itumie kama mtaji huku ukijipanga kwa mwaka mwingine wa masomo,kwani kwa mwaka huu naona itakuwa ngumu kwako,hiyo laki moja ukiamua kuuingiza kwenye biashara ndani ya mwaka itakuwa pesa ndefu sana.
Nimekushauri hivyo kutokana na uzoefu wangu,mimi mwenyewe nimesoma kwa mfumo kama wako,nilipomaliza masomo ya kidato cha sita miaka ile nilishindwa kuendelea kwa changamoto kama yako, nilikaa mwaka mzima nikipambana na maisha na mwaka uliofuata nilijiunga na diploma ya ualimu kwa kujilipia mwenyewe maanana kwa mwaka mmoja niliokaa uraiani nilitengeneza almost 2M so hiyo niliutumia kulipa karo na mahitaji ya chuo.
Lakini pia waweza jishughulisha na shughuli za ujenzi ukianza kama msaidizi wa fundi,kazi hii nayo nimeifanya sana wakati wa likizo zangu za chuo,nimechanganya sana zege na matofali ya cement nimefyatua sana,kwa kazi hizo enzi zile nilikuwa nalipwa elfu 5000+ na hakika nilikuwa napata sana hela, kwa likizo nzima nilikuwa najikuta Nina kama 300,000+,chuo nilichosoma mimi, wanachuo wengi walijua mimi natoka kwa familia ya kitajiri kumbe haikuwa hivyo,
Mwanamme kupambana mkuu,pambana usikate tamaaa,kila la kheli.