Msaada wenu tafadhali wanaJF, maji yamezidi unga

Econometrician

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2013
Posts
17,815
Reaction score
33,486
Habari zenu ndugu wana JF,

Ndugu zangu nimepata na matatizo ambayo yanahitaji kuyatatua kwa uharaka,ninahitaji Mkopo wa Milioni 1.

Mkopo nitarejesha ndani ya miezi 2 kwa awamu 2,nitafurahi kama nitapata kwa riba ya 10%-15% kwa mwezi. Dhamana niliyonayo ni mshahara wangu wa kila mwezi.
 
Kuna member humu natamani nimtag akusaidie, sema atajua tu mie ndo nimekulengesha kwake.
Angekupa bila riba na huenda ungerudisha nusu tu.
Anasaidia sana watu
 
Takukuru watakukamata hiyo ya kukabdhi kadi kwa Mkopeshaji hairusiwi!!
Takukuru wanakamata wale ambao pesa zao zina ushirirkina, yaani hata uchakarike kwa sarakasi gani deni hulipi na riba inazidi kubwa. Kama habari ya juzi ya yule mstaafu, alikopa 10M jamaa wakachukua 25M.
 
Pesa gani tena jaman si tuli kubaliana adi zipite siku 21
 
Mama Samia anayajua haya lakini
 
Sasa hapo miezi miwili inabidi 30% interest

Ingekuwa kwa 1 month ingependeza 20%

Ni hayo tu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…