Msaada wenu: Nina mikakati nataka ninunue nyumba Mbezi beach

Msaada wenu: Nina mikakati nataka ninunue nyumba Mbezi beach

faru joni

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
478
Reaction score
734
Habarini za asubuhi, pole na majukumu ya kujenga taifa pendwa la Tanzania
.
.
Niende kwenye mada moja kwa moja
.
.
Mimi ni kijana umri wangu (range 20--25)
.
.
Elimu yangu ni degree moja (Bsc)
.
.
Kiihistoria nimezaliwa kwenye familia duni kabisa, ila historia ya babu yangu alikuwa na Mali nyingi sana zilikuja kusambaratika baada ya yeye kufariki, sikukuta kitu chochote katika kuzaliwa, na kukua kwangu..tumeishi maisha ya tabu mno ila nashukuru mungu kwa kumalizia elimu yangu na kujitambua vyema.
.
.
Dhumuni kuu la Uzi huu ni
.
.
Katika kukuwa kwangu akuna kitu nimetoka kukipenda kwenye maisha yangu kama kuwa na nyumba nzuri ya kuishi, nimekuwa nikivutiwa sana sana (niseme kupitia maelezo) kuishi MBEZI BEACH, ndoto zangu zote siku za usoni niwe na nyumba uko.
.
.
Nimekuwa nikiwauliza watu wengi sana kuhusina na mbezi beach upatikanaji wa nyumba ili niweze kutimiza malengo yangu, naishia kukatishwa tamaa, kuwa kule bei sana ata uchange pesa za ukoo wako wote hautaweza nunua kule nk.
.
.
Kwa sasa sina kazi maalum ya kupata pesa zaidi ya pesa ya kula, na ndio nimemaliza chuo mwaka huu.
.
.
Naombeni mkakati thabiti kabisa ata shamba niende nikajichimbie uko.. kikubwa ndoto yangu itimie tu,
.
.
Naombeni uchanganuzi wenu, ujuzi wenu na mawazo yenu thabiti kuhusina na izi ndoto zangu za siku za usoni
.
.
Mungu awabariki sana sana
 
mkakat namba moja hakikisha unatunisha akaunti yako ya benki.

awazo mbadala kuna sehemu nyingine za kuishi nzuri sio lazima huko mbezi ila kwakua umedhamiria na ni shauku yako ya muda mrefu basi Mungu akufanyie wepesi uoate hitaji lako na utimize ndoto zako
 
Mkuu unajua lolote kuhusu forex? Huku watu wanavuna mapesa yaani hutomaliza mwaka utakuwa umetimiza ndoto zako!!!
 
1. Jitahidi uwe mwizi upate zaidi ya pesa ya kula. 2. Kama hutaki kuwa mwizi, fanya biashara ili upate pato la ziada uongeze na kile unachotunza/kubaki kwenye mshahara wako. 3. Uwe na nidhamu ya fedha ndoto yako itatimia.
 
1. Jitahidi uwe mwizi upate zaidi ya pesa ya kula. 2. Kama hutaki kuwa mwizi, fanya biashara ili upate pato la ziada uongeze na kile unachotunza/kubaki kwenye mshahara wako. 3. Uwe na nidhamu ya fedha ndoto yako itatimia.
Nimekuelewa mkuu, katika mambo matatu uliyo-ni-orodheshea yapo ntakayoyachukua mungu akubariki sana
 
Nashukuru sana kwa michango yenu naendelea kupokea maoni,mapendezo yenu waungwana..
 
kaka sasa hivi unazipata kwa bei nzuri tu cha msingi pitia page za instagram za madalali utaona,Ukianza tu kazi funga mkanda utafikia lengo lako usikate tamaa kabisa
 
Asante sana ndugu yangu, mungu akubariki sana
kaka sasa hivi unazipata kwa bei nzuri tu cha msingi pitia page za instagram za madalali utaona,Ukianza tu kazi funga mkanda utafikia lengo lako usikate tamaa kabisa
 
Konki Konki Konki master, oil chafu.List ya Tatu inatoka lini?
 
Kwa hela ya kuajiriwa huwez nunua nyumba huko bro otherwise uwe fisadi
 
Back
Top Bottom