Huo si ushauri ndg yangu, mwenzako amepatwa na tatizo anaomba ushauri wewe unamkatisha tamaa? nadhani sio ustaarabu. Jaribu kujiweka katika mazingira aliyonayo, halafu ujibiwe hivyo wewe ungejisikiaje? mpe ushauri si kumkatisha tamaa, leo kwake kesho kwako!!!Niuzie ukanunue shamba ulime na kufuga, biashara hiyo hauiwezi na kagari kako kamoja.
Asante sana mkuu.Nakushauri kwanza piga chini dereva na tingo wake, chukua rafiki yako awe dereva then pata mzigo kwa kutumia njia anazotumia yeye then nenda/safiri na gari mpaka Tunduma say x2 au 3 hivi hapo tayari utapata picha isiyo na chenga chenga, kamwe usijaribu kwenda naye kwani atakutupia misala yote njiani, atakulengesha kila mahali palipo na muzani, kwa matrafiki etc, ali mradi akuonyeshe kwamba anapata shida sana, sikubaliani na kiasi cha diseli inayotumika na hapo kama utasafiri naye basi atakufix vizuri tu utakapoenda kulala asubuhi yake utasaga meno, kwa ujumla watu wengi siku hizi hawana heshima na kazi ila wiziwizi tu
Wana JF naomba mnisaidie katika hili . Nina lori linafanya biashara za kusafirisha mizigo kwenda mikoani. Lakini toka limeanza kufanya biashara faida yake haionekani. Kwenda na kurudi mapato ni milion mbili, matumizi ni diesel huwa kwenye mil. 1.5, udalali na upakiaji ni laki moja. mizani ni kama elfu arobaini na allowance ya dereva ni laki hamsini. najikuta kama nabakiwa na laki mbili, na hapo lazima nitoe hela ya lubricants, matengenezo madogomadogo. Sasa nikipiga mahesabu naona hamna faida kwani gari likitakiwa matengenezo makubwa najikuta naenda kuchukua hela ya mshahara kutengeneza, hapo bado kodi mbalimbali za TRA, SUMATRA, n.k.
Naomba mtu mwenye uwezo wa kuendesha hii biashara anisaidie kuisimamia ikibidi kutafuta soko zuri .
Niuzie ukanunue shamba ulime na kufuga, biashara hiyo hauiwezi na kagari kako kamoja.
Wana JF naomba mnisaidie katika hili . Nina lori linafanya biashara za kusafirisha mizigo kwenda mikoani. Lakini toka limeanza kufanya biashara faida yake haionekani. Kwenda na kurudi mapato ni milion mbili, matumizi ni diesel huwa kwenye mil. 1.5, udalali na upakiaji ni laki moja. mizani ni kama elfu arobaini na allowance ya dereva ni laki hamsini. najikuta kama nabakiwa na laki mbili, na hapo lazima nitoe hela ya lubricants, matengenezo madogomadogo. Sasa nikipiga mahesabu naona hamna faida kwani gari likitakiwa matengenezo makubwa najikuta naenda kuchukua hela ya mshahara kutengeneza, hapo bado kodi mbalimbali za TRA, SUMATRA, n.k.
Naomba mtu mwenye uwezo wa kuendesha hii biashara anisaidie kuisimamia ikibidi kutafuta soko zuri .
Msaada wenu wana JF ni mkubwa sana napata faraja kuwa member wa JF. Nawashukuru sana wote muliochangia kwa moyo mmoja