Hehehe ati aliens, msiwe mnakimbilia alien, mungu, na vitu vingine sijui mnavyotoa wapi, ukikosa explanation ya kitu uliza tulia, mambo ya alien unajipotezea muda tu na kupumbaza wengine.
Aliyekwambia simu hazitengenezwi na binadamu nani? Nimesomea haya mambo na nishashiriki project moja ya kampuni kubwa sana duniani ya utengenezaji simu (siitaji) nilihusika kutengeneza SSD. Huwezi enda chuoni ukafundishwa kutengeneza simu mwanzo mwisho sababu sio rahisi kihivyo, simu ni kitu complex sana, simu moja unaweza kuta inamikono ya watu zaidi ya 2,000, naongelea hardware tu. Mfano team yetu tuliyokua tunadeal na part moja tu ya SSD tulikua watu 20. hapo sio SSD nzima, ni part moja tu. Kila mtu kaspecialize kwenye jambo flani, in short hamna anayeweza tengeneza mwenyewe kila kiungo hadi ikakamilika, ila kuassemble anaweza mtu moja.
Vifaa vingi vya electronics ambavyo ni complex kama simu na computers ndo vinavyotengenezwa hivyo, ni mikono ya binadamu tu, japo zile very small transistors tunatumia machine (ambazo pia zimetengenezwa na binadamu), unafanya formulation nzima kwenye software, then unatupa kwenye machine tu inachapa kazi unapata board yako safi kabisa inayofanya unachotaka.
Tatizo la watanzania wengi moja, mnahisi wafundi simu na tv mtaani ni watu waliosomea computer science au electronics engineering, hehehe! hiyo kazi nilikua naifanya toka nina miaka 10, inahitaji internet tu kujua kila kitu, watu wanaounda hizi machine hawapo mtaani wanachomachoma boards, wapo kwenye big companies wanapiga mzigo.