Msaada: Wanaojua mambo ya LUKU

Msaada: Wanaojua mambo ya LUKU

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,270
Katikati ya mwezi wa tisa mwaka huu, niliomba kufungiwa Luku.TANESCO walikubali ombi langu wakanifungia mita ya LUKU, ikiwa na units 50.

Mwezi wa kumi katikati nilipoona units zimebaki 5 tu, nikenda kwa wakala kuongeza.Nilimpa wakala sh 5,000 ununuzi wa units akanipa risiti yenye namba za kuingiza kwenye luku.Nilipoingiza namba hizo, units 6 zikaongezeka.

Juzi tarehe 5/11/2015 saa za jioni nikahitaji kuongeza units, hivyo nikatumia njia ya m-pesa.Nilituma sh 5,000 zikakataliwa kwamba hazitoshi.Baadaye nikatuma sh 8,000.Nikapokea jibu toka LUKU2 kwamba nimepewa units 3.5KWH.

Tarehe 5,6, matumizi yangu ya umeme yalikuwa makubwa sana hivyo leo jumamosi 7/11/2015 nikaamua kuongeza units.Nikatumia m-pesa tena kiasi kilekile cha sh 8,000.Jibu likaja toka LUKU2 kwamba nimepata units 22.1KWH.

Kwa wale mnaoelewa naomba mnisaidie maswali yangu haya:

1. Kwa nini sh 5,000 zilikataliwa kwamba hazitoshi (na btw walinirudishia)
2. Kwa nini elf nane ya mwanzo ilileta units 3.5kwh na ya pili 22.1kwh?
 
Ngoja wataalam waje wakupe majibu
 
Kwanza hizo unit50 huwa ni mkopo unazilipa baadaye
Pili elfu tano ilikataliwa sababu ulikuwa huwezi kulipa service charge.
Tatu unit zimeongezeka kutokana ulikuwa umelipa makato...
 
Kweli kuuliza sio ujinga! Hata wakikucheka, ushatoa ujinga, utakuwa mjanja wa luku
Elf 5 ya mwanzo ilikataliwa kwa sbb ulitakiwa kulipia service charge around 6000, na unalipia hiyo service charge kila mwanzo wa mwezi, ukishalipia hiyo ndo hela zinazobaki unanunua units zako, ndo maana elf 8 ya pili ulipata units nyingi zaidi manake hukuwa na deni tena!
so unapoanza mwezi unatakiwa utoe at least elf 10 ili upate units za kutosha, then waweza hata kuwa unanunua units za buku 2 mbili, note hiyo service charge n kila mwezi, so hata usipotumia umeme mwezi mzima, next month utadaiwa service charge ya miez mi2! So n bora kulipa kila mwez kuepuka machungu
 
Umejibiwa vema sana na wadau waliotangulia hapo juu mkuu SHIEKA, isipokuwa kwa jambo moja tu ambalo hata mimi sijakupata vema bado kutokana na maelezo yako ya utangulizi uliyoyatoa hapo juu, kwamba ulipofanya manunuzi yako ya kwanza ulianza kwa kutoa shs. 5,000= na ukaweza kununua units za umeme kabla ya kukatwa gharama ya zile unit 50 za mkopo ulizofungiwa nazo na mita??
Maana kwa kawaida ulitakiwa ukatwe kwanza kiasi cha kama Tshs. 18,900= hivi kabla ya kuruhusiwa kuanza kuuziwa umeme, hivyo labda ni kama TANESCO walijisahau kukuingizia hilo deni kwa ajili ya hizo unit 50 za awali, otherwise mi nakuhakikishia lazima watakuja kukukata huko mbeleni siku wakilikumbuka, so nikaona nikupe angalizo la mapema ndugu yangu ili ujiandae na kwa hili pia.

Asanteni nyote kwa kunisikiliza.
 
Service charge tu. Ata ukiangalia kwenye risiti utaona wameandika ..
 
kiti kingine kunatarrif group watumiaji wa kawaida ni tarrif 4 ambavyo kiwango cha manununuzi ya unit ni kidogo ila tanesco wanafanya makusudi wanawaunganisha wateja wao tarrif 1 ambalo ni kundi mahsusi kwa watumiaji wakubwa wa umeme inabidi uende tanesco uangalie wamekuweka group la tarrif gani kama wamekuweka tarrif 1 waambie wakubadilishe kwenda tarrif 4
 
Kweli kuuliza sio ujinga! Hata wakikucheka, ushatoa ujinga, utakuwa mjanja wa luku
Elf 5 ya mwanzo ilikataliwa kwa sbb ulitakiwa kulipia service charge around 6000, na unalipia hiyo service charge kila mwanzo wa mwezi, ukishalipia hiyo ndo hela zinazobaki unanunua units zako, ndo maana elf 8 ya pili ulipata units nyingi zaidi manake hukuwa na deni tena!
so unapoanza mwezi unatakiwa utoe at least elf 10 ili upate units za kutosha, then waweza hata kuwa unanunua units za buku 2 mbili, note hiyo service charge n kila mwezi, so hata usipotumia umeme mwezi mzima, next month utadaiwa service charge ya miez mi2! So n bora kulipa kila mwez kuepuka machungu

Tahadhari kulipa fedha nyingi. kuna jamaa yangu alimkodishia TX nyumba yake, yule mzungu kwa kujihadhari usumbufu wa kulnunua LUKU kila mwezi akanunua umeme wa Shs. 1.2mil. Baada ya miaka miwili yule mzungu akamaliza mkataba wake na akarudisha nyumba kwa mwenyewe. Jamaa akaona aishi mwenyewe kwenye nyumba yake. Alipohamia akakuta zimebaki kama unit 200 hivi, jamaa meno nje akajua atasevu umeme kwa miezi minne. Siku umeme ulipokwisha kwenda kulipa LUKU aliipata, fikiria service charge ya miaka miwili na nusu.
Hivyo kama unanunua umeme mwingi, basi kila mwezi lipa kama Shs. 6000/= ukwepe kilichompata jamaa yangu.
 
Back
Top Bottom