Kwa vile binaadamu sote ni wenye kufanya makosa kila siku kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
(كل بني آدم خطاء، و خير الخطائين التوابون)) حسن الألباني صحيح الجامع)
(Kila Binaadamu ni mkosa na mkosa mbora kabisa ni yule anayeomba toba)).
Kwa Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) hata binaadamu awe ana makosa vipi, huenda akafutiwa dhambi zake zote, kwa hiyo mtu asikate tamaa au kukhofu kuwa dhambi zake hazitofutwa.
(قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ))
(Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao, msikate tamaa na Rahma ya Allaah. Hakika Allaah husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)) Az-Zumar: 53
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuamrisha tumuombe toba katika Aayah nyingi za Qur-aan kama mfano wa Aayah zifuatazo:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))
(Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah toba iliyo ya kweli)) [At-Tahriym: 8]
(وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ)
(Na tubuni nyote kwa Allaah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa)) [An- Nuur: 31]