Msaada wakuu vyuo vya kilimo na mifugo tanzania

Patrioxylic

Member
Joined
Jan 8, 2018
Posts
44
Reaction score
9
Habari wana jf anayevijua vyuo vizuri vya kilimo na mifugo ngazi ya diploma na kozi Zinazotolewa msaada tafadhari.
 
Nenda Ukirigulu elimu itolewayo hutajutia kusoma Kilimo na Mifugo Mkuu! Tena pale itachukua general agricultural yaani Kilimo na Mifugo kwa mwaka mmoja! Lakini kama umesoma certificate miaka miwili! Ila kama ni form six unatakiwa upige miaka miwili pale
 
Kuhusu mifugo watembelee wakala wa mafunzo ya mifugo yaani ''livestock training agency'' (LITA) kupitia www.lita.go.tz na kuhusu kilimo watemebelee watu wa MATI (Ministry of Agriculture Training Institute).

Hao LITA wanashughulika na mafunzo ya mifugo na shughuli za maabara za tiba-wanyama tu, wanatoa mafunzo kupitia kwenye kampasi zao kadhaa zilizopo maeneo mbalimbali nchini, Nani mafunzo ni kwa ngazi ya astashahada (certificate) na stashahada (diploma).

MATI wao watakufundisha kilimo-mazao kwa maana ya crop production, kilimo-jumla au kilimo mchanganyo yaani general agriculture (mifugo na uzalishaji mazao pamoja), na pia wanatoa kozi maalum za umwagiliaji na matumizi ardhi. Mafunzo hayo yanatolewa pia kwa ngazi za astashahada na stashahada kupitia kampasi zao mbalimbali.

Mafunzo ni ya muda wa miaka miwili kwa ngazi ya certificate na diploma ni ama ya miaka miwili au mwaka mmoja kutegemeana na kama umetoka kidato cha sita (utasoma miwili) au una certificate (utasoma mmoja).

Kwa ujumla vigezo ni ufaulu kwenye masomo ya sayansi kama ambavyo wanakuwa wameainisha kwenye fomu za maombi kwa kila mwaka wa masomo. Mhitimu wa kidato cha nne anasoma certificate na yule wa kidato cha sita au mwenye certificate tayari anasoma diploma.

Namna ya kuomba, unajaza fomu za maombi ambazo huwa wanazitoa muda wa kupokea maombi ukifika (mara nyingi fomu hutolewa kupitia tovuti zao), unaambatanisha na viambatanisho muhimu vyote watakavyoeleza kuvitaka kisha unawatumia kwa njia ya posta.

Karibu sana kwenye sekta ya kilimo.

NB: Maelezo haya yasikusababishie kushindwa kutembelea tovuti za taasisi hizo kama nilivyokushauri hapo juu. Kule ninaamini utapata mengi zaidi.

Kila la heri.
 
Kama umesoma form six diploma ni muda gani na je kwa aliyetokea form four
 
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom