Msaada wa wataalam

Kachera

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2018
Posts
372
Reaction score
274
Habari naombeni ushauri. Mimi Ni baba wa watoto watatu. Wa Kwanza miaka nane wa pili miaka mi nne huyu watatu ndio anaenda miezi miwili. Changamoto niliyo nayo huyu wa tatu amegoma kuengeza kilo alizaliwa na kilo 3.3 baada ya wiki sita amepelekwa clinic haja ongeza kilo zimebaki hizo alizo zaliwa nazo kwa wajuzi msaada.ila wenzake walivyo zaliwa hawakua na changamoto hiyo asnteni.
 
Ondoa wasiwasi mkuu. Hiyo ni kawaida.

Kikawaida mtoto aliyezaliwa hupungua uzito kwa takribani 10% ya ule uzito aliozaliwa nao. Hii inatokea katika ile wiki ya kwanza (siku 7) kwa sababu mtoto akizaliwa anakuwa na maji mengi, hivyo kupungua kwake uzito inasababishwa na kupungua kwa hayo maji mwilini.

Kisha anaanza kuurudisha uzito alioupoteza ndani ya wiki 2 au 3 baadae, kwa kuwa atakuwa akiongezeka 15g-20g kwa siku.

Kwa hesabu rahisi tu, mtoto wako kama alizaliwa na 3.3kg, wiki yake ya kwanza alipoteza 10% ya uzito wake (0.33kg- kiasi alichopoteza), hivyo akabakiwa na kilo 2.9kg. Kisha akaanza kugain weight kwa 15g-20g per day kwa wiki 5 zilizobaki (siku 35) akaongezeka 0.5kg.
Kwahiyo tunategemea baada ya wiki 6 uzito wake uwe: 2.9kg+0.5kg= 3.4kg

Hizo ni estimation tu, sio lazima iwe exactly that weight.
 
Na wameniambia hawawezi kumpatia chanjo mpaka
atakapo fikisha kilo tano kwenda juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…