Kwanza nikupongeze kwa wazo zuri na tofauti ulilolifikiria.
Binafsi napendezwa sana na fashion hususani kuanzisha brands, logo, na lebo kwa ujumla, na siri kubwa iliyonifanya nipende hii fashion design ni kutokana na mm kuweza kuwa mchoraji na ilishangia watu kunishauri nianze kufanya biashara ya nguo ikiwemo brands, logo, hata lebo pia, wengine walinishauri nikasomee graphic design.....
Naomba nikujibu maswali yako.
1. Ndio uwezo wa kuprinti nguo inawezekana ila kwa hapa Tanzania wapo ila kiwango chao ni kidogo hivyo inahitajika uagize mashine za kuprinti ambazo gharama zake ni kuanzia milioni 10 mpaka milioni 15. Ila kumbuka inahitajika upate mbunifu au wewe mwenyewe uwe mbunifu wa kudesign na printini iwe kiwango chenye ubora.
2. Gharama au mtaji wa kuanzia kufanya hiyo biashara inaweza ikawa kwenye milioni 30 na zaidi. nikiiwa na maana ya kwamba kununua mashine ya kuprinti, rangi, na baadhi ya vifaa na nguo inategemea unataka pea ngapi..??
3. Kwa hapa Tanzania nadhani zipo sehemu ambazo wanafanya biashara ya kuprinti na mfumo wa utengenezaji hata kudizaini nguo ila ubora na kiwango chao ni kidogo mno.
Hivyo basi kutengeneza au kudesign nguo kwa nchi mbali mbali za ughaibuni inahitaji uwe na mtaji mkubwa sana
Kwa mfano: unataka kuanzisha brand label ama logo ya nguo na kuipa jina ( MKARUKA SHOES WEAR & MKARUKA CLOTH LINE ) hii itakugharimu pesa nyingi mno kutengeneza jina lako na bidhaa kuuzika itakuwa ngumu.
FANYA MAMBO HAYA KATIKA MFUMO MZIMA WA KUTENGENEZA AU KUANZISHA BRANDI, LEBO, LOGO YA NGUO, VIATU N.K
1. Andaa mtaji wa kutosha ili kuanzisha hii biashara ya kutengeneza nguo. Mtaji huo kwa makadirio usiwe chini ya milioni 50 au milioni 70.
2. Tafuta kampuni ya utengenezaji wa nguo , viatu , mabegi , n.k
Na uweke share na kampuni hiyo kutokana na makubaliano yenu.
3. Tafuta watu wabunifu au wewe mwenyewe uwe mbunifu katika kutengeneza bidhaa yako na iweze kuwateka wateja wako ili bidhaa yako iweze kununuliwa na kuvutia pia, graphic designer na hata wachoraji wanaweza wakawa moja kati ya watu wa kukupa wazo na ubunifu mkubwa katika kutengeneza bidhaa yako.
4. Hakikisha bidhaa yako inakuwa na ubora na mvuto wa hali ya juu ili kumfanya mteja kuipenda na iwe unauzika katika soko.
5. Ili bidhaa yako iuzike kirahisi itakubidi utafute kampuni au duka la nguo maarufu au mtu maarufu aweze kuitangaza biashara yako.
Mfano: unaweza ukatengeneza bidhaa yako kupitia kampuni ya nike au adidas na kuitangaza kupitia mtu maarufu kama ycee au diamond platnumz. Hii ni kulingana na mapato yako kama inaruhusu,
6. Bei yako ya bidhaa iwe poa ili kila mteja aweze kununua na kuridhika na kile anachouziwa.
* * kwa mtazamo wangu ni vyema ukajipanga na ni vizuri uende afrika ya kusini ( south Africa ) wana nguo nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu. Na kumbuka kwamba south Africa wanatengeneza nguo zao wenyewe na ni nadra sana nguo kutoka nchi nyingine kuingia katika soko la afrika ya kusini,
Sio lazima uende China, marekani, uingereza, ufaransa, n.k
* * * pia katika kudesign nguo zako jaribu kuwa tofauti na za wabongo mfano: nguo ya W.C.B au african boy inaonekana ni t-sheti imeprintiwa kawaida hivyo tizama nguo ya mwanamuziki tyga kampuni yake ya LAST KINGS ( L K ) alivyo design kwa ubora na kiwango haionekani kama hizi za kwetu za kibongo.
Nakutakia mafanikio mema..
** 2017 loading___________