MSAADA WA USHAURI; Ninataka Kuanzisha Brand Ya Nguo Kama Ilivyo WCB Wasafi, Nike, Puma, Yeezy N.K

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,620
34,053
Habarini Wadau Wa Jukwaa Hili,

- Mimi Ninavutiwa Sana Haya Masuala Ya Fashion - Sasa Nimefikiria Kuanza Mradi Wangu Rasmi Wa Mavazi Kama Nilivzotaja Hapo Juu, Naomba Mwenye Kujua Abc Za Haya Mambo Anisaidie.

- Zaidi Naomba Kujua Kuhusu Mambo Yafuatayo;

1.Je, Naweza Kuprint Nguo Bora Kabisa Aina Zote Kama Hoods, Viatu, Kofia, Socks, Mabegi, Majinsi Nk Hapa Hapa Tanzania - Na Kama Ni Hapa Ni Maeneo Gani Wanapatikana ?

2.Je, Gharama Za Kuanzia Inaweza Kuwa Kama Kiasi Gani ?

3.Je, Kama Hakuna Kwa Hapa Tanzania Inatakiwa China, Naweza Pata Abc Za Utaratibu Ukoje ?

4.Mambo Mengine Unayojua Unayoweza Kunisaidia ?

Nitashukuru Kwa Msaada
 
Wengi wanaanza kwa kuuza brand kubwa duniani kwaajili ya kuwa familiar na trend ya soko na masuala yanayohusiana na biashara hiyo.Pia wanatumia muda huo kuanza kujenga Brand zao.

Kisha taratibu wanaanza ku-establish clothing line zao kwa kuzingatia hali ya soko.

Wanaofanikiwa ni wale ambao wameshajenga msingi mzuri wa wateja, yaani tayari wana majina makubwa sokoni(wameshajibrand).

Bdozen ~ Born to Shine
Jux ~ African Boy
Kidoti ~ Kidoti bags
Robby One - Robby One fashion

Otherwise uwe na mtaji mkubwa kutosha kuwekeza katika production na marketing ili uingie moja kwa moja na brand yako.
 
Watanzania kuvaa brand zao bado ni tatizo mkuu, hao WCB wanainfluence kubwa kwenye industry lakini cloth line yao sidhani kama inauzwa kulingana na matarajio yao.
Ni Kweli Sister Usemacho - Lakini Ndio Ujasiriamali, Kujaribu Mambo Mapya.Hata Hivyo Kwa Hapa Tanzania Kuna Hao Wasafi, Chui Chui, Born To Shine Nk.Na Idea Yangu Pamoja Na Niche Niliyoichagua Na Jinsi Nilivyojipanga Naamini Nitafanikiwa Kama Nitapata Hizo Abc Chache
 
Wengi wanaanza kwa kuuza brand kubwa duniani kwaajili ya kuwa familiar na trend ya soko na masuala yanayohusiana na biashara hiyo.Pia wanatumia muda huo kuanza kujenga Brand zao.

Kisha taratibu wanaanza ku-establish clothing line zao kwa kuzingatia hali ya soko.

Wanaofanikiwa ni wale ambao wameshajenga msingi mzuri wa wateja, yaani tayari wana majina makubwa sokoni(wameshajibrand).

Bdozen ~ Born to Shine
Jux ~ African Boy
Kidoti ~ Kidoti bags
Robby One - Robby One fashion

Otherwise uwe na mtaji mkubwa kutosha kuwekeza katika production na marketing ili uingie moja kwa moja na brand yako.
Nashukuru Sana Kwa Ufafanuzi Wako Mkuu, Mfano Kwa Hao Uliowataja Hapo Juu Wanafanyia Wapi Production Yao Kama Unafahamu ?
 
Nashukuru Sana Kwa Ufafanuzi Wako Mkuu, Mfano Kwa Hao Uliowataja Hapo Juu Wanafanyia Wapi Production Yao Kama Unafahamu ?
China is a favorite manufacturing destination for clothing brands because of its cheap production costs. In China, you may be able to get up to 90% off the costs of production compared to producing in other countries. But since you don’t live in China but in a different continent entirely,

The question comes: how do you get a reliable and trusted clothing manufacturer in China?

Wengi wanazalisha products zao China, lakini sifahamu specifically Manufacturers wanaofanya nao kazi.Angalau unaweza kuanzia hapo kufanya research
 
Naona Kibongobongo Hakuna Watengenezaji Hususani Wa Hoods Na Viatu
 
Ndugu hongera na usikate tamaa ingawa majibu mengi yanayotolewa humu yanaashiria kuwa kitu kama hicho hakiwezekani,Inawezekana kabisa,maana zipo brand ambazo zimewahi Kuwa na coverage kubwa hasa zinazohusu masuala ya fashion ila nahisi kama wenyewe hawakuwa serious walifanya hasa just for funny,mfano wanaume family,walikuwa wanauza nguo zao hasa chupi mpaka vijijini huko,ni brand ambayo ilipokelewa vizur sana,nyingine ni kama Weusi,na Leo WCB, mkubwa mi nahisi inawezekana ila cha kwanza anzisha maduka au ofisi ambazo utauza nguo na Ku design hilo jina husika mfano Mkaruka fashion,hakikisha ni sehem ambayo kuwe kuna kila bidhaa ya fashion inayovutia kwa sasa,then tumia media kulitangaza jina na ikiwezekana Ku host baadhi ya matamasha nk,mfano beach festivals nk,usikate tamaa kufanya HVO ndani ya miaka kadhaa brand yako itakuwa kubwa sana,ila hakikisha kila unacho ki design kiwe kwenye quality ya hali ya juu usikubali brand yako itumike kutengeneza vitu chini ya kiwango,nk utafanikiwa nothing impossible
 
Kwanza nikupongeze kwa wazo zuri na tofauti ulilolifikiria.
Binafsi napendezwa sana na fashion hususani kuanzisha brands, logo, na lebo kwa ujumla, na siri kubwa iliyonifanya nipende hii fashion design ni kutokana na mm kuweza kuwa mchoraji na ilishangia watu kunishauri nianze kufanya biashara ya nguo ikiwemo brands, logo, hata lebo pia, wengine walinishauri nikasomee graphic design.....

Naomba nikujibu maswali yako.

1. Ndio uwezo wa kuprinti nguo inawezekana ila kwa hapa Tanzania wapo ila kiwango chao ni kidogo hivyo inahitajika uagize mashine za kuprinti ambazo gharama zake ni kuanzia milioni 10 mpaka milioni 15. Ila kumbuka inahitajika upate mbunifu au wewe mwenyewe uwe mbunifu wa kudesign na printini iwe kiwango chenye ubora.


2. Gharama au mtaji wa kuanzia kufanya hiyo biashara inaweza ikawa kwenye milioni 30 na zaidi. nikiiwa na maana ya kwamba kununua mashine ya kuprinti, rangi, na baadhi ya vifaa na nguo inategemea unataka pea ngapi..??

3. Kwa hapa Tanzania nadhani zipo sehemu ambazo wanafanya biashara ya kuprinti na mfumo wa utengenezaji hata kudizaini nguo ila ubora na kiwango chao ni kidogo mno.
Hivyo basi kutengeneza au kudesign nguo kwa nchi mbali mbali za ughaibuni inahitaji uwe na mtaji mkubwa sana
Kwa mfano: unataka kuanzisha brand label ama logo ya nguo na kuipa jina ( MKARUKA SHOES WEAR & MKARUKA CLOTH LINE ) hii itakugharimu pesa nyingi mno kutengeneza jina lako na bidhaa kuuzika itakuwa ngumu.

FANYA MAMBO HAYA KATIKA MFUMO MZIMA WA KUTENGENEZA AU KUANZISHA BRANDI, LEBO, LOGO YA NGUO, VIATU N.K

1. Andaa mtaji wa kutosha ili kuanzisha hii biashara ya kutengeneza nguo. Mtaji huo kwa makadirio usiwe chini ya milioni 50 au milioni 70.

2. Tafuta kampuni ya utengenezaji wa nguo , viatu , mabegi , n.k
Na uweke share na kampuni hiyo kutokana na makubaliano yenu.

3. Tafuta watu wabunifu au wewe mwenyewe uwe mbunifu katika kutengeneza bidhaa yako na iweze kuwateka wateja wako ili bidhaa yako iweze kununuliwa na kuvutia pia, graphic designer na hata wachoraji wanaweza wakawa moja kati ya watu wa kukupa wazo na ubunifu mkubwa katika kutengeneza bidhaa yako.

4. Hakikisha bidhaa yako inakuwa na ubora na mvuto wa hali ya juu ili kumfanya mteja kuipenda na iwe unauzika katika soko.

5. Ili bidhaa yako iuzike kirahisi itakubidi utafute kampuni au duka la nguo maarufu au mtu maarufu aweze kuitangaza biashara yako.
Mfano: unaweza ukatengeneza bidhaa yako kupitia kampuni ya nike au adidas na kuitangaza kupitia mtu maarufu kama ycee au diamond platnumz. Hii ni kulingana na mapato yako kama inaruhusu,

6. Bei yako ya bidhaa iwe poa ili kila mteja aweze kununua na kuridhika na kile anachouziwa.

* * kwa mtazamo wangu ni vyema ukajipanga na ni vizuri uende afrika ya kusini ( south Africa ) wana nguo nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu. Na kumbuka kwamba south Africa wanatengeneza nguo zao wenyewe na ni nadra sana nguo kutoka nchi nyingine kuingia katika soko la afrika ya kusini,
Sio lazima uende China, marekani, uingereza, ufaransa, n.k

* * * pia katika kudesign nguo zako jaribu kuwa tofauti na za wabongo mfano: nguo ya W.C.B au african boy inaonekana ni t-sheti imeprintiwa kawaida hivyo tizama nguo ya mwanamuziki tyga kampuni yake ya LAST KINGS ( L K ) alivyo design kwa ubora na kiwango haionekani kama hizi za kwetu za kibongo.

Nakutakia mafanikio mema..
** 2017 loading___________
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom