Msaada wa ushauri/Nasaha..

Al Adawi

Member
Feb 25, 2011
91
38
Habari zenu wana Jamvi :;
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka na rehema zake kwangu. Kwa ufupi nimepitia ktk kipindi cha majaribu..iko. hivi, :Nilikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na dada fulani, ambao mie niliuona ni serious relationship,ambayo nilitegemea kunifikisha kwenye ndoa, if God wished. Nilimaliza degree yangu hapo mlimani miaka miwili ilopita;baadaye nilikwenda Italy kwa masters yangu..kabla ya kusafiri nilianzisha uhusiano na dada fulani aliyekuwa anamalizia degree ya medicine,na kwakweli nilimpenda na niliamini naye alinipenda. Kwa kipindi chote nilipokuwa chuoni huko tuliwasiliana na nilimtumia pesa nyingi tu kuliko hata nilivyowatumia ndugu zangu. Nilivyorudi mwanzoni mwa mwaka huu, alikuwa kesha badilika kimwenendo na tabia., akawa ni mtu wa kupenda kujirusha, kwenda night clubs hata nikimuonya hanielewi tena. Kwahakika hata life standard and stile yake ilibadilika kutokana na pesa nilizokuwa nikimtumia. Muda si mrefu nikapata habari kuwa anauhusiano wa kimapenzi na kijana fulani ati anafanya ikulu. Nilifuatilia nikapata uhakika. Niliumia sana na katika harakati za kutaka arudishe gari dogo nililomnunulia, nilimfata Moshi alikokuwa amekwenda, ofcourse nilimfata huko baada ya kusikia kuwa akirudi dar atakaa siku moja then atakuwa safarini China. Basi nilikwenda huko na akanikimbia, niliamua kurudi. Nilipofika maeneo ya Korogwe nilipata ajali mbaya ya gari na niliponea chupuchupu kwani gari yangu ilikuwa ikiwaka moto ndipo walitokea wasamaria wema wakanichomoa. Yule dada alipata taarifa yeye na hata wazazi wake, lakini kwakipindi chote nilichokuwa hospitalini sikuwahi pokea hata SMS ya kunipa pole. Ndugu zangu imefikia hatua sasa sitaki kujikubali na hali hii. Nimejitahidi kusamehe na kusahau, lakini ninashindwa.ukweli nahitaji msaada wa ushauri na faraja ya wote walioguswa na mkasa huu.
 
Mkuu yameshatokea just sahau na na endelea na maisha yako
hapo hakuna kitu na hakuna mwanamke wa kukufaa katika huyo dada
Mwache na pambana kujenga maisha yako kwa sasa ufanye na utafute wa kukufaa
Huyo ndio hivyo ni ndege aliye mtini hakufai
 
 
 
 
 
Potezea 2 mkuu..mtoto wa kike asikufanye uone maisha yako hayana thaman tena,piga moyo konde na life litasonga 2.
 
 
 
 
 
Pole kwa uliyopitia,lakini mshukuru Mungu wako kwani atakuwa amekuepushia balaa kubwa zaidi. Anza kujipanga upya na utafanikiwa tu.
 
 
Mwanamke yeyote ambae sio mkeo wa ndoa
ni risk ambayo una take kama mwanaume,kupata au kukosa ni matokeo.....

Kwanza unapaswa kushukuru umemjua kabla hujamuoa......

Halafu zawadi ukishampa mtu ,hasa kwenye mapenzi,sio vizuri kudai.....hata kama gari....
 
msichana najichana hivo we bado unamkumbuka pamoja na ajali mbaya yote hiyo uliyopata na huwezi jua labda mchawi alitaka ufe, pole sana jipe muda utapona maumivu na kupata msichana wa ndoto zako, mpaka ilipofikia huyo msichana wala ha deserve kuwa na wewe kabisa, gari kitu gani, mwachie tu kaka angu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…