akatanyukuile
JF-Expert Member
- Sep 13, 2019
- 314
- 308
Vipo ila nimelazimika kusimamisha ujenzi kwa kuhofia kuingia hasara. Na kwanini wananinyima vibari vya ujenzi? Sasa nichukue hatua zip ?Kama aliyekuuzia yupo na hana wasiwasi na ulifata taratibu zote za manunuzi basi huwezi kupigwa ila hao jamaa wanatengeneza mazingira ya kukupiga..mashahidi wapo pande zate mbili ? Muuzaji na mnunuzi na mihuri ya serikali ?
Kwamba hakuna mtu anaye kuja na kudai eneo ni lake bali ni viongozi wanasema kuwa kuna mgogoro? Acha uoga andika barua ikidai wakupe kibali cha ujenzi na peleka nakala kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya. Subiri majibu. Labda watamleta huyo wanayesema anadai eneo ni lake. Akija deal naye na huyo aliyekuuziaVipo ila nimelazimika kusimamisha ujenzi kwa kuhofia kuingia hasara. Na kwanini wananinyima vibari vya ujenzi? Sasa nichukue hatua zip ?
Mkuu akatanyukuile, kwanza nakupa pole kwa jambo lako linalokusibu. Mkuu, mgogoro wa ardhi hausemwi tu na kiongozi au mkaxi wa mtaa lilipo eneo. Anayedai ni kwake anapaswa kukulalamikia kwa mujibu wa taratibu zilizopo ikiwemo kuwasilisha mgogoro wake kwenye Baraza la Ardhi lenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Nakushauri uendelee na hatua za kupata kibali cha ujenzi(kama ni lazima) na uendelee na ujenzi. Ukiona unapigwa danadana kwenye kupata kibali hicho, fuata ngazi za kiserikali kupata haki yako ya kibali. Kimsingi, kibali ni mambo ya kiserikali na kuna ngazi nyingi za kiserikali za kutatua jambo lako.
Ikitokea kuna anayedai mahali ulipopanunua ni kwake, atamlalamikia aliyekuuzia, anayedai amemuuzia na wewe kutaka atangazwe kuwa ni mmiliki halali. Mgogoro ukianza mtasikilizwa na ukweli utapatikana. Kwasasa hakuna mgogoro hapo, kuna harufu ya utapeli na ubabaishaji.
Jiridhishe takwa la kibali cha ujenzi na uchukue hatua nilizozianisha hapo juu. Tena, ujuandae kwa huduma ya Wakili kama mgogoro wa ardhi utaibuka. Kila la kheri Mkuu!
Mwifwa
Sawa mkuu,Kwamba hakuna mtu anaye kuja na kudai eneo ni lake bali ni viongozi wanasema kuwa kuna mgogoro? Acha uoga andika barua ikidai wakupe kibali cha ujenzi na peleka nakala kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya. Subiri majibu. Labda watamleta huyo wanayesema anadai eneo ni lake. Akija deal naye na huyo aliyekuuzia
acha uoga jenga hapo, we muoga ttzSawa mkuu,