Msaada wa ushauri (mambo ya sheria)

akatanyukuile

JF-Expert Member
Sep 13, 2019
314
308
Habari za mda huu wana jamvi mm sijambo na mungu ameonesha utukufu wake.

Bila kuwachosha ninaomba nijikite kwenye mada lengwa. Mimi ni kijana ambaye bado ninahangaika na maisha. Nimefika mjini kama kimbilio langu baada ya kuhitimu chuo 2015 kada ya ualimu na kukosa ajira. Sikubweteka nilijitosa mtaan ili niweze kujikwamua mimi pamoja familia yangu inayonitegemea kwa asilimia kadhaa.

Mimi ninakaa kinondoni tegeta, nilipo zichanga kwa takiribani mwaka na unusu niliweza kupata pesa kiasi cha milioni tatu na nusu hiv ambazo zilikua kwenye account yangu bila kazi. Wazo likanijia nn nifanye na pesa yangu hiyo, niliweza kupata ushauri wakasema ninunue kiwanja angalau niweze kuanza ujenzi hata kama kitakua chumba kimoja ila kingelitosha kwani hali ya kukodi ni ngumu bora niwe kwenye kibanda changu.

Tatizo linakuja kwenye kiwanja hicho, niliponunua nilikua makini ilibidi wauzaji niwapeleke selikari za mitaa ambao kiuhalisia ndio wamekasimishwa madaraka ya kusimamia aridha kwenye mitaa yao.

Tangu ninunue yapata mwaka sasa na miezi kadhaa, sikuawai kuona mtu anakuja kudai eneo ni lake, nimekua nikifanya shughuli tofauti bila bugudha, juzi kati tu ndipo nilipopata vijisent kadhaa nikasema sasa ni wakati wa kuweka kajumba japo kadogo ila kangeniondolea adha ya kodi.

Niliweka msigi nikiwa katikati kwenye ujenzi wakaja vijana waliojitambulisha wanatokea katani yaani ni watendaji ndani ya office ya katibukata hivo wakaniomba vibali vya ujenzi, nilikua sina hivo wakasema itabidi nisimamamishe ujenzi nianze taratibu za kutafta vibali hivyo.

Nilitii sheria na kuanza ufuatiliaji wa vibali nikawaomba wanisaidie taratibu zip zinaanza kufatwa, waliweza kuniambia yakua zipo form zinapatikana office ya mtendaji kata kwa shillingi laki mbili kama fain ya kuanza ujenzi bila taratibu. Kwavile nilikua na nia ya kujenga sikusita nikaitoa kwa huyo afisa, na kuniruhusu kuendelea na kutafuta watu wa kusain maeneo yao wakiwemo afisa mtendaji wa kijini pamoja na diwani kata. Mziki ndipo ukaanza nilipo peleka kwa afisa aligoma kusain na kudai eneo langu lina mgogoro, nikawaomba wanipe chanzo cha mgogoro hawakunipatia ila nikiwaambia wanisainie hawataki wanadai eneo lilishauzwa hivo nimepigwa. Mpaka ninapoandika hapa sielewi nianzie wapi,

Maombi, ninajua jukwaa hili ni penyewe, mnisaidie nifate taratibu zipi kwani nimeishajawa na woga ninashindwa kuendelea na baadae mwenye eneo akaja kama wanavo dai , pili mm nitamshitaki nani hapo kwani aliyeniuzia anadai nani amekusumbua na sina la kumjibu, hivo nilikua ninaomba mnisaidie ikiwezekana wale wanaousiika na aridhi tuwasiliane ili mnipe mwanga maana ninaona ninaelekea kudhurumiwa,

Kiwanja kipo mabwe pande mtaa wa mbopo,. Ninaomba mnisamehe kwa kuandika maelezo marefu sana ila nikatika hali ya kuwaweka saw hali ninayoipitia.
Karibu.
 
Kama aliyekuuzia yupo na hana wasiwasi na ulifata taratibu zote za manunuzi basi huwezi kupigwa ila hao jamaa wanatengeneza mazingira ya kukupiga..mashahidi wapo pande zate mbili ? Muuzaji na mnunuzi na mihuri ya serikali ?
 
Vipo ila nimelazimika kusimamisha ujenzi kwa kuhofia kuingia hasara. Na kwanini wananinyima vibari vya ujenzi? Sasa nichukue hatua zip ?
 
Vipo ila nimelazimika kusimamisha ujenzi kwa kuhofia kuingia hasara. Na kwanini wananinyima vibari vya ujenzi? Sasa nichukue hatua zip ?
Kwamba hakuna mtu anaye kuja na kudai eneo ni lake bali ni viongozi wanasema kuwa kuna mgogoro? Acha uoga andika barua ikidai wakupe kibali cha ujenzi na peleka nakala kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya. Subiri majibu. Labda watamleta huyo wanayesema anadai eneo ni lake. Akija deal naye na huyo aliyekuuzia
 
Dah! kuna mambo yanasikitisha sana... kuna watu siyo waaminifu kabisa...

Ngoja waje kukupa muongozo...

Cc: mahondaw
 
Mkuu akatanyukuile, kwanza nakupa pole kwa jambo lako linalokusibu. Mkuu, mgogoro wa ardhi hausemwi tu na kiongozi au mkazi wa mtaa lilipo eneo. Anayedai ni kwake anapaswa kukulalamikia kwa mujibu wa taratibu zilizopo ikiwemo kuwasilisha mgogoro wake kwenye Baraza la Ardhi lenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Nakushauri uendelee na hatua za kupata kibali cha ujenzi(kama ni lazima) na uendelee na ujenzi. Ukiona unapigwa danadana kwenye kupata kibali hicho, fuata ngazi za kiserikali kupata haki yako ya kibali. Kimsingi, kibali ni mambo ya kiserikali na kuna ngazi nyingi za kiserikali za kutatua jambo lako.

Ikitokea kuna anayedai mahali ulipopanunua ni kwake, atamlalamikia aliyekuuzia, anayedai amemuuzia na wewe kutaka atangazwe kuwa ni mmiliki halali. Mgogoro ukianza mtasikilizwa na ukweli utapatikana. Kwasasa hakuna mgogoro hapo, kuna harufu ya utapeli na ubabaishaji.

Jiridhishe takwa la kibali cha ujenzi na uchukue hatua nilizozianisha hapo juu. Tena, ujiandae kwa huduma ya Wakili kama mgogoro wa ardhi utaibuka. Kila la kheri Mkuu!

Mwifwa
 
Mkuu akatanyukuile, kwanza nakupa pole kwa jambo lako linalokusibu. Mkuu, mgogoro wa ardhi hausemwi tu na kiongozi au mkaxi wa mtaa lilipo eneo. Anayedai ni kwake anapaswa kukulalamikia kwa mujibu wa taratibu zilizopo ikiwemo kuwasilisha mgogoro wake kwenye Baraza la Ardhi lenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Nakushauri uendelee na hatua za kupata kibali cha ujenzi(kama ni lazima) na uendelee na ujenzi. Ukiona unapigwa danadana kwenye kupata kibali hicho, fuata ngazi za kiserikali kupata haki yako ya kibali. Kimsingi, kibali ni mambo ya kiserikali na kuna ngazi nyingi za kiserikali za kutatua jambo lako.

Ikitokea kuna anayedai mahali ulipopanunua ni kwake, atamlalamikia aliyekuuzia, anayedai amemuuzia na wewe kutaka atangazwe kuwa ni mmiliki halali. Mgogoro ukianza mtasikilizwa na ukweli utapatikana. Kwasasa hakuna mgogoro hapo, kuna harufu ya utapeli na ubabaishaji.

Jiridhishe takwa la kibali cha ujenzi na uchukue hatua nilizozianisha hapo juu. Tena, ujuandae kwa huduma ya Wakili kama mgogoro wa ardhi utaibuka. Kila la kheri Mkuu!

Mwifwa

Mkuu hapo kwenye huduma ya Wakili naona kama kubiashara zaidi!! Au ni huduma ya msaada wa wakili?
 
Kwamba hakuna mtu anaye kuja na kudai eneo ni lake bali ni viongozi wanasema kuwa kuna mgogoro? Acha uoga andika barua ikidai wakupe kibali cha ujenzi na peleka nakala kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya. Subiri majibu. Labda watamleta huyo wanayesema anadai eneo ni lake. Akija deal naye na huyo aliyekuuzia
Sawa mkuu,
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom