Msaada wa tiba ya Amiba sugu

JOESKY

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
816
2,032
Ndugu zangu natanguliza salam zangu kwenu!

Nimekuwa nikipata shida ya amiba mara kwa mara nimetumia dawa kama Tinidazole kwa nyakati tofauti tofauti na namaliza dozi lakini bado tatizo linarudia tena.

Naomba mnishauri kulingana na uzoefu wenu wa kitabibu kuhusu huu ugonjwa.

Napaswa nitumie dawa gani ya uhakika wa kumaliza tatizo?

Asanteni.
 
1.Hiyo amoeba ilikua diagnosed vipi na wapi? Huwa unapata dalili zipi na kufanyiwa kipimo kipi (na wapi) kuambiwa una amoeba?

2.Huwa unamaliza dozi ya dawa unazoandikiwa?

3.Ni kwamba baada ya kutumia dawa unapata nafuu, kisha baada ya muda (muda gani?) unaanza kupata tena upya hizo dalili, au ni kwamba dawa hazijawahi kukupa nafuu yoyote?- Hapo kuna mawili, kwamba ni kweli shida ni amoeba, kinachotokea ni unapata amoeba, unatibiwa vizuri na kupona, kisha unaendelea na tabia zako zile zile hatarishi zilizokufanya upate amoeba (eg kunywa maji yasiyochemshwa, kula chakula kilichopoa au ambacho hakijapikwa vizuri, kula chakula/matunda bila kunawa mikono, kupenda kula kachumbari ambayo huna uhakika kama nyanya zake zilioshwa vizuri na kwa usahihi, etc etc); So,hapo inakua hakuna namna zaidi ya kupata amoeba upyaaaa, AU hiyo sio amoeba bali ni tatizo la tumbo ambalo linahitaji ufanyiwe vipimo beyond stool analysis kujua shida na upatiwe matibabu stahiki (hasa kama huwa hupati nafuu yoyote hata baada ya kutumia dawa).

Ushaur wangu:
Kwa maoni yangu, kitu cha kwanza kwa sasa hivi cha muhimu kabisa ni kudetermine je, kinachokusumbua ni amoeba kweli? Na hapa ni lazima na muhimu uonwe na kuwa attended na daktari bingwa (wa magojwa ya ndani-physician) kwenye hospitali ya rufaa yenye uwezo wa kufanya vipimo beyond stool analysis (vipimo kama stool culture,etc kulingana na dalili zinazokukabili).

Pole sana mkuu. Wahi haraka hospitali ya rufaa ya mkoa au hospitali ya kanda yenye physician upate muafaka. Ni muhimu sana hii...Unaweza ukawa kila siku unatibiwa "amoeba" ambayo haipo kumbe una tatizo kubwa kwenye utumbo linaendelea kukukula tuu (naongea hivi kwa uzoefu wangu-mtu anatibiwa amoeba miaka na miaka haponi, kumbe ana saratani au uvimbe kwenye utumbo).
JOESKY
 
1.Hiyo amoeba ilikua diagnosed vipi na wapi? Huwa unapata dalili zipi na kufanyiwa kipimo kipi (na wapi) kuambiwa una amoeba?
2.Huwa unamaliza dozi ya dawa unazoandikiwa?...
Nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu. Nimejifunza kitu kutoka kikubwa sana kutokana na hii comment yako. Nitalifanyia kazi hili jambo kwa uhakika zaidi. Nimependa sana aina yako ya utoaji ushauri mkuu ubarikiwe.

Unajua kwa maisha yetu haya ya kiafrika ni tatizo kubwa sana kwa magonjwa haya yatokanayo na uchafu (kinyesi). Ninapokuwa nimepata tiba au dawa ya amiba unafuu unapatikana na ninaendelea vizuri shida inakuwa kama ulivgoeleza hapo juu kuzingatia usafi na ulaji wa vyakula.

Dalili zote ni za amiba na ninapokuwa nimepima nambiwa ni amiba huwa naamini nina amiba sugu kumbe tatizo linaanzia kwenye mazingira hayahaya ninayoishi kutozingatia usafishaji matunda kabla ya kula kuchemsha maji ya kunywa kula chakula cha baridi nk.

Asante sana
 
Ndugu zangu natanguliza salam zangu kwenu!

Nimekuwa nikipata shida ya amiba mara kwa mara nimetumia dawa kama Tinidazole kwa nyakati tofauti tofauti na namaliza dozi lakini bado tatizo linarudia tena.

Naomba mnishauri kulingana na uzoefu wenu wa kitabibu kuhusu huu ugonjwa
Napaswa nitumie dawa gani ya uhakika wa kumaliza tatizo???

Asanteni!!!
Amiba sugu siku hizi haisikii Vidonge jaribu sindano ikishindikana tutafute wataalam wa dawa za asili ili tupate kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole.
 
Hakuna amiba sugu, kati ya wadudu rahisi kufa bac amiba ni mojawapo. Shida ni pale ukienda hospital/maabara unataka aone kile ww unachofikilia kama kama umeenda private bac jua hawana mamlaka yakugeuza mtazamo wako ingia apige pesa uende.

Lakn amiba ni hatar isipotibiwa, kwan inaweza sababisha majipu kwenye ini.

Ushauli kafanye culture ili ujue best na sensitive na
 
Asante sana ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom