James Mhangwa
JF-Expert Member
- Feb 3, 2017
- 609
- 513
Habari za wakati huu madaktari wa JF?
Tafadhali naomba msaada wa haraka, mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 ninasumbuliwa na ugonjwa wa hernia kwa muda mrefu japo dalili nimezibaini November mwaka jana.
Nilifanyiwa vipimo wiki mbili zilizopita nikaelezwa kuwa ugonjwa umekuwa sugu na kinachohitajika ni upasuaji.
Hivi sasa nipo Mwanza na natarajia kusafiri kesho kuelekea Arusha kwa ajili ya zoezi hilo.
Sasa kinachonichanganya sana, ni kwamba tangu jana kila mtu ninayeongea naye ananishauri nitumie dawa za kienyeji kwa madai kwamba upasuaji unasababisha ugumba, eti kuna uwezekano mkubwa sana wa kukosa mtoto.
Je madai haya ni kweli? Na madaktari mnanishauri vipi?
Karibuni...