Msaada wa sheria za mtandaoni

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,013
7,164
Wakuu mambo vipi? Sheria zinasemaje kama mtu anapost picha zako fb na kuandika maneno ya udhalilishaji.... ? Hatua gani ya kwanza natakiwa kufanya ? Au naweza kumfungulia kesi mahakamani?
 
Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mitandao kifungu cha16 (Cyber Crime Act) Taarifa ama chapisho lolote (kwenye mfumo wa kompyuta) lenye lengo la kudhalilisha, kutukana, kutisha, kudanganya ama kupotosha uma ni kinyume cha sheria. Sheria imeweka adhabu ya kifungo si chini ya miaka mitatu au faini si chini ya milioni tano au vyote kwa pamoja dhidi ya yoyote atayekutwa na hatia.

Sheria hii ni ya jinai hivyo taratibu na mwenendo wa mashitaka hufuata kama makosa mengine ya jinai ambapo jamuhuri huendesha mashitaka.
 
Pamoja na hayo unaweza kumripoti huyo mtu Facebook kwa bullying akafungiwa jumla.
 
Back
Top Bottom