Nikusaidie kidogo hapo pekundu, pinus ni jina la jumla. Ni vizuri ukataja jina kamili la huo ukoo wa pinus. Hata mivinje inaangukia ktk ukoo wa pinus.
Kwa ukanda wa Mfindi,Kilolo,Njombe na Makete, pinus patula aka pines ndio maarufu, ukienda kwa Bwana miti ye yote ni vizuri ukampa jina kamili. Pili kuna spacing hujazungumzia kabisa, je eka hiyo unataka ipandwe 3M x 3M au unataka ipandwe 2.5M x 3M na eka yako ni ya 70m x 70m au ya vipi. Kama ni 3 x 3 ktk eka moja ya ukubwa wa 70 x 70 utakuwa na miche 529 hivi, hapa hujaweka fireline space.
Ukitumia 2.5M x 3M kwa eka hiyo hiyo unaweza panda/otesha miti mpaka 600. Kipimo hiki cha 2.5m x 3m hakifai kwa mkulima anayemaanisha kwa sababu hutoa mazao mabaya wakati wa kuvuna. Kwa kule Iringa ni vijiji vichache sana vyenye ardhi yenye uwezo wa miti kutoa mbao ktk miaka hiyo, sehemu kubwa ni zaidi ya miaka 10.