Kuna rafiki yangu mmoja alifunga ndoa zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, hivi majuzi alinidokeza kwamba tangu afunge ndoa na mke wake alijisikia furaha ya ndoa katika wiki ya kwanza tu na baada ya hapo hakupata tena kuifurahia ndoa yake. Kwa mtizamo wake ni kwamba ilikuwa ni baada ya hiyo wiki moja ndipo alipokuja kugundua kwamba aliyeoa hakuwa chagua la moyo wake.
Binafsi, nilishituka sana nilipomsikia akinisimulia jambo hili. Mshangao wangu ulitokana na ukweli kwamba wakati alipokuwa ktk mchakato wa kufunga nae ndoa mimi nilikuwa pamoja nae muda mrefu. Nakumbuka enzi zile alikuwa akija na picha za mchumba wake (mke wake kwa sasa) ofisini! Ilikuwa kila alipopata nafasi, angezichukuwa picha za mchumba wake na kuanza kuziangalia. Angeweza kuzikodolea macho picha hizo hadi robo saa jambo ambalo baadae hata mimi alianza kunikera! Pale nilipomuuliza ni kwanini kila wakati anapenda kuziangalia picha za mchumba wake tena kwa muda mrefu hivyo hadi wakati mwingine alikuwa anaacha kufanya kazi kwa muda kwa kuziangalia picha hizo; jibu lake kila mara lilikuwa ni kv anampenda sana hivyo kila wakati anapenda kumwangalia na haishi hamu kuziangalia picha hizo! Hata hivyo, leo hii ananiambia kwamba ilimchukua wiki moja tu kufurahia ndoa yake jambo lililomfanya amrejee mpenzi wake wa zamani ambae alikuwa ameishi nae zaidi ya miaka mitano! Rafiki yangu amechanganyikiwa na hajui afanye nini hasa ukizingatia kwamba dini yake hairuhusu kuacha mke na yeye bado ni kijana mdogo sana ambae hajafikisha hata miaka 30! Mshikaji wangu huyu aliniomba msaada wa mawazo kuhusu afanye nini, nami nawageukia wana jamvi kutafuta msaada wa mawazo.

Inawezekana huyo mkewe alimuendea mumewe kwa kalumanzila ili aolewe sasa ndio yameisha hivyo. Maana tunaweza mlaumu mbaba hapa kumbe aliingizwa mkenge

kazi ipo hizi ndio za siku hizi maruweruwe kibao zinaitwa bora ndoa
hahhaaa.....expaya date reached...!!Inawezekana huyo mkewe alimuendea mumewe kwa kalumanzila ili aolewe sasa ndio yameisha hivyo. Maana tunaweza mlaumu mbaba hapa kumbe aliingizwa mkenge
kaka,labda ungechelewa kidogo mimi ningepost uzi kama huu kwa asilimia tisini....mimi pia nina rafiki yangu wa karibu sana,mwaka 2009,masaa machache kabla ya send off yeye akiwa ndio mtarajiwa,akinipa habari kama hiyo,sikuamini na nikamwambia acha utani,alisisitiza lakini yakaisha na siku mbili baadaye akafunga ndoa ya kanisani,katoliki!wamekaa na mkewe kama mwaka hivi,wamepata mtoto lakini hivi ninavyoandika,amemwacha mkewe wa ndoa na anataka kuoa mwingine!!mke kahangaika mpaka kwa wazazi wa jamaa,wameshindwa kusawazisha,mimi pia nimejaribu kunusuri hiyo ndoa kwa nafasi yangu,nimeshindwa!!jamaa yuko shinyanga na mkewe wa ndoa yuko moshi......sielewi,nini kinatokea juu ya hali hii,nahisi inaanza kushika kasi,tujadiliane kwa pamojaKuna rafiki yangu mmoja alifunga ndoa zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, hivi majuzi alinidokeza kwamba tangu afunge ndoa na mke wake alijisikia furaha ya ndoa katika wiki ya kwanza tu na baada ya hapo hakupata tena kuifurahia ndoa yake. Kwa mtizamo wake ni kwamba ilikuwa ni baada ya hiyo wiki moja ndipo alipokuja kugundua kwamba aliyeoa hakuwa chagua la moyo wake.
Binafsi, nilishituka sana nilipomsikia akinisimulia jambo hili. Mshangao wangu ulitokana na ukweli kwamba wakati alipokuwa ktk mchakato wa kufunga nae ndoa mimi nilikuwa pamoja nae muda mrefu. Nakumbuka enzi zile alikuwa akija na picha za mchumba wake (mke wake kwa sasa) ofisini! Ilikuwa kila alipopata nafasi, angezichukuwa picha za mchumba wake na kuanza kuziangalia. Angeweza kuzikodolea macho picha hizo hadi robo saa jambo ambalo baadae hata mimi alianza kunikera! Pale nilipomuuliza ni kwanini kila wakati anapenda kuziangalia picha za mchumba wake tena kwa muda mrefu hivyo hadi wakati mwingine alikuwa anaacha kufanya kazi kwa muda kwa kuziangalia picha hizo; jibu lake kila mara lilikuwa ni kv anampenda sana hivyo kila wakati anapenda kumwangalia na haishi hamu kuziangalia picha hizo! Hata hivyo, leo hii ananiambia kwamba ilimchukua wiki moja tu kufurahia ndoa yake jambo lililomfanya amrejee mpenzi wake wa zamani ambae alikuwa ameishi nae zaidi ya miaka mitano! Rafiki yangu amechanganyikiwa na hajui afanye nini hasa ukizingatia kwamba dini yake hairuhusu kuacha mke na yeye bado ni kijana mdogo sana ambae hajafikisha hata miaka 30! Mshikaji wangu huyu aliniomba msaada wa mawazo kuhusu afanye nini, nami nawageukia wana jamvi kutafuta msaada wa mawazo.
:smile-big:tatizo la jamaa ni kufanya comparison ya mkewe na huyo kipwepwelepwe cha nje ajitahidi kurudisha moyo kwa yf