Sasa ka ndo umemaliza waweza fanya kati ya yafuatayo kujipima kama kweli umeelewa.
1. Site mtu anaupload picha ya vyakula vya kitanzania alafu kwenye backend yako inafanya processing kwa AI na kusema chakuna ni labda wali nyama, na kumpa details zote mfano estimate ya protein ni kiasi flani per 100g e.t.c
- Hapa unaweza tumia tensorflow ukatrain model kwa picha mbalimbali ya vyakula then ukarudi kwenye php yako kutengeneza backend.
2. Fanya mapping ya Dar es salaam, njia zote za hayo magari ya public, map vituo mbalimbali then tengeneza ramani, mtu akiingia kwenye site mfano yupo mwenge anataka kwenda sehemu flani, unamuonyesha aende kituo flani, apande bus flani, ikifika sehemu flani afanye transfer kwenda bus linalokwenda sehemu flani hadi anafika anapohitaji kwa haraka zaidi.
- Hapa utahitaji usome graph datastructure, ujue utafanyeje mapping, ujue kila kituo utakiweka vipi, weight e.t.c alafu pia shortest path algorithms zipo kadhaa, ipi itafaa kwa situation ipi.
3. Tengeneza a real time collaborating IDE online, coder anaweza ingia online akaanza kuandika code, kunakua na syntax highlighting kabisa, alafu anakua na link akishare na mtu yeyote huyo mtu anaweza join wakafanya collaboration in realtime, yaani kila anachoandika moja na mwingine anaona wakati huohuo kama kwenye google docs vile, unaweza pendezesha na kuweka thumbnails au jina
- Hapa itakulazimu kutumia real time tools kama socket.io
4. Rahisi zaidi, real time voting system, watu wanaweza piga kura, hapa itabidi udeal sana na unazuia vipi bots, unazuia vipi same person voting multiple times, how do you secure it. Alafu inatakiwa iwe realtime, yaani watu 10 wakifungua browser zao moja akivote basi namba inapanda kwa wote bila kurefresh.
- Hapa pia itakulazimu uguse either socket.io au mqtt
Nikifikiria project nyingine simple simple ntaongeza hapa.